超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Rais Xi asema ziara yake kupeleka uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Peru kwenye ngazi mpya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 15, 2024

Rais wa China Xi Jinping akikaribishwa kwa furaha na Waziri Mkuu wa Peru Gustavo Adrianzen na maofisa wengine waandamizi  baada ya kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kijeshi wa Callao huko Lima, Peru, Novemba 14, 2024. (Xinhua/Li Xueren)

Rais wa China Xi Jinping akikaribishwa kwa furaha na Waziri Mkuu wa Peru Gustavo Adrianzen na maofisa wengine waandamizi baada ya kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kijeshi wa Callao huko Lima, Peru, Novemba 14, 2024. (Xinhua/Li Xueren)

LIMA - Rais Xi Jinping wa China amesema Alhamisi kwamba anaamini kwa juhudi za pamoja za pande zote mbili, ziara yake hii itapeleka uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa China na Peru kwenye kiwango kipya, kuhimiza ushirikiano kati yao kupata matokeo halisi katika setka mbalimbali.

Katika taarifa yake ya maandishi iliyotolewa baada ya kuwasili Lima, Peru, Rais Xi amesema anaona furaha kubwa kufanya ziara ya kiserikali kwa mara nyingine tena katika Jamhuri ya Peru na kutokana na mwaliko wa Rais Dina Boluarte, na kuhudhuria Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya APEC, na anahisi kuwa karibu sana na Peru baada ya kufika tena nchi hii tajiri yenye ardhi nzuri na historia ndefu.

Akiwa kwa niaba ya serikali ya China na wananchi wake, Rais Xi ametoa salamu za dhati za kutakia kila la kheri kwa serikali ya Peru na wananchi wake.

Rais Xi amesema, urafiki kati ya China na Peru ulianzia enzi na dahari, na umekita mizizi sana katika mioyo ya watu, mapema zaidi ya miaka 400 iliyopita, watu wa nchi hizo mbili walianza kufanya mawasiliano ya kirafiki kwa kupitia Njia ya Hariri ya Baharini na "The Manila Galleons," au "La Nao de China."

China na Peru zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia miaka 53 iliyopita, ikiifanya Peru kuwa moja ya nchi za kwanza za Latini Amerika kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya Watu wa China, amesema.

Rais Xi amesema, katika miaka ya hivi karibuni, kwa juhudi za pamoja za sekta mbalimbali za nchi hizo mbili, uhusiano kati ya China na Peru yamepata maendeleo siku hadi siku, na hali ya kuaminiana kisiasa imeimarishwa zaidi, nchi hizo mbili zimeelewana na kuungana mkono juu ya masuala yanayohusu maslahi ya msingi na mambo makubwa yanayofuatiliwa na kila mmoja wao.

Rais Xi ameongeza kuwa anatarajia kuhudhuria Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa kiuchumi ya APEC na kufanya juhudi pamoja na pande zote ili kuhakikisha mafanikio ya mkutano huo na kutoa mchango mpya kwa ajili ya kujenga uchumi wa uwazi wa Asia Pasifiki, kuhimiza ukuaji wa uchumi wa dunia, na kujenga kwa pamoja jumuiya ya Asia Pasifiki yenye mustakabali wa pamoja.

Rais Xi alipofika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kijeshi wa Callao huko Lima, alikaribishwa kwa furaha na Waziri Mkuu wa Peru Gustavo Adrianzen na maofisa wengine waandamizi. Mwanafunzi wa Peru alitumia lugha ya Kichina kwa kumkaribisha Rais Xi. Askari wa gwaride walijipanga pande zote mbili za zulia jekundu kutoa salamu ya heshima.?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha