Lugha Nyingine
Rais Xi asema kutarajia kuimarisha zaidi uhusiano kati ya China na Brazil
Rais Xi Jinping wa China akiwasili Rio de Janeiro kwa kuhudhuria kwenye Mkutano wa Kilele wa 19 wa Viongozi wa G20 na ziara ya kiserikali nchini Brazil kutokana na mwaliko wa Rais Luiz Inacio Lula da Silva, Novemba 17, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
RIO DE JANEIRO - Rais wa China Xi Jinping amesema anatarajia kubadilishana mawazo kwa kina na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva juu ya kuimarisha zaidi uhusiano kati ya China na Brazil, kuhimiza kuoana kwa mikakati ya maendeleo ya nchi hizo mbili, na masuala ya kimataifa na kikanda yanayofuatiliwa nao kwa pamoja.
Rais Xi ameyasema hayo siku ya Jumapili katika taarifa yake ya maandishi alipowasili Brazil kwa kuhudhuria kwenye Mkutano wa Kilele wa 19 wa Viongozi wa G20 na kufanya ziara ya kiserikali nchini humo kutokana na mwaliko wa Rais Lula. Rais Xi pia ametoa salamu za dhati za kutakia kila la kheri kwa serikali ya Brazil na watu wake.
Rais Xi amesema kuwa aliwahi kutembelea Brazil mara nne na kujionea maendeleo na mabadiliko nchini humo katika miaka 30 iliyopita, anahisi kuwa karibu sana na Brazil anapoingia tena katika nchi hii yenye hamasa kubwa na uchangamfu.
Rais Xi amesema, China na Brazil ni marafiki wenye nia moja na matarajio sawa, na ni washirika wazuri wanaosonga mbele bega kwa bega, ingawa zimetenganishwa kwa bahari, China na Brazil, nchi mbili kubwa zinazoendelea katika pande za mashariki na magharibi mwa dunia mtawalia, zinavutiana na kuitikiana kwa mbali.
Katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo mbili zimeendelea kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa, kupata matokeo katika ushirikiano wa kivitendo, kupata mafanikio ya ushirikiano katika mambo ya kitamaduni, na kuonyesha uhai mpya wa nyakati katika urafiki wa jadi, Rais Xi amesema.
China na Brazil pia kwa pamoja zimetoa sauti ya haki ya Nchi za Kusini kwenye jukwaa la kimataifa na kutoa mchango muhimu kwa ajili ya kuhimiza amani na maendeleo ya dunia, Rais Xi ameongeza.
Mwaka huu wakati China na Brazil zikiadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, uhusiano kati ya nchi hizo mbili uko katika hatua muhimu ya kihistoria ya kusonga mbele kwenye msingi wa mafanikio yaliyopatikana.
Rais Xi amewasili Brazil kutoka Lima, Peru ambapo alihudhuria kwenye Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya APEC na kufanya ziara ya kiserikali nchini Peru.?
Rais Xi Jinping wa China akiwasili Rio de Janeiro kwa kuhudhuria kwenye Mkutano wa Kilele wa 19 wa Viongozi wa G20 na ziara ya kiserikali nchini Brazil kutokana na mwaliko wa Rais Luiz Inacio Lula da Silva, Novemba 17, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
Watu wakimkaribidha Rais Xi Jinping wa China huko Rio de Janeiro, Brazil, Novemba 17, 2024. (Xinhua/Li Yan)
Watu wakimkaribisha Rais Xi Jinping wa China huko Rio de Janeiro, Brazil, Novemba 17, 2024. (Xinhua/Li Yan)
Watu wakimuaga Rais Xi Jinping wa China akiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege wa Lima, Peru, Novemba 17, 2024. (Xinhua/Bi Xiaoyang)

people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma