超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Rais Xi Jinping ahutubia mkutano wa 31 wa viongozi wa APEC

(CRI Online) Novemba 18, 2024

(Picha/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu isemayo "Kubeba Wajibu wa Nyakati Zetu na Kuhimiza kwa Pamoja Maendeleo ya Asia na Pasifiki" kwenye Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya APEC uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Lima cha Peru, Novemba 16, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Picha/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu isemayo "Kubeba Wajibu wa Nyakati Zetu na Kuhimiza kwa Pamoja Maendeleo ya Asia na Pasifiki" kwenye Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya APEC uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Lima cha Peru, Novemba 16, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China amehutubia mkutano wa 31 wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia Pasifiki (APEC) siku ya Jumamosi mjini Lima nchini Peru, akitoa wito kwa nchi za Asia-Pasifiki kubeba majukumu yao na kuhimiza kwa pamoja maendeleo ya eneo la Asia-Pasifiki wakati ambapo ushirikiano wa eneo hilo unakabiliana na changamoto mbalimbali kutokana na siasa za kijiografia, msimamo wa upande mmoja na sera za kujihami kibiashara.

Rais Xi amependekeza kujenga muundo wenye uwazi na muunganisho wa ushirikiano kati ya nchi za Asia-Pasifiki, akisema kuwa pande husika zinapaswa kuendelea kufuata mwelekeo wa uchumi wazi na mfumo wa ushirikiano wa pande nyingi, kushikilia kithabiti mfumo wa biashara wa pande nyingi huku Shirika la Biashara Duniani (WTO) likiwa msingi wake, kuamsha kikamilifu wajibu wa APEC kama kiatamizi cha kanuni za uchumi na biashara duniani, na kuhimiza mafungamano ya kiuchumi na muunganisho wa kikanda.

Rais Xi, pia ametoa wito wa kubomoa kuta zinazozuia mtiririko huru wa biashara, uwekezaji, teknolojia na huduma, kuhakikisha utulivu na ufanisi wa minyororo ya viwanda na ugavi, na kuhimiza mzunguko wa kiuchumi katika kanda ya Asia-Pasifiki na dunia kwa ujumla.

Aidha, Rais Xi ametoa wito wa kuhimiza ubunifu wa kijani kama msukumo wa ukuaji wa uchumi wa Asia-Pasifiki, akiongeza kuwa China inaendeleza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora kwa kuzingatia hali yake halisi na kuimarisha ushirikiano na pande husika katika ubunifu wa kijani.

Amesema pande zote husika zinahitaji kutumia vizuri fursa zinazoletwa na awamu mpya ya mapinduzi ya kisayansi na mageuzi ya kiviwanda, na kuimarisha mabadilishano na ushirikiano katika sekta za akili mnemba, teknolojia ya Quantum Information, maisha na afya, na sekta nyingine nyingi za mstari wa mbele.

Amesema, China itazindua Pendekezo la Ushirikiano wa Mabadilishano ya Data Duniani, na kutafuta ushirikiano wa kina na pande mbalimbali ili kufanya mabadilishano hayo yawe salama, rahisi na yenye ufanisi.

Rais Xi pia amependekeza kujenga dhana ya maendeleo ya Asia-Pasifiki yaliyo jumuishi na yanayonufaisha wote, akitoa wito kwa pande husika kutumia vyema jukwaa la APEC, kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kiufundi, na kuongeza uungaji mkono kwa nchi zinazoendelea na nchi zilizo nyuma kiuchumi, ili matunda ya maendeleo yanufaishe nchi nyingi zaidi na watu wengi zaidi.

Rais Xi amesema kuwa maendeleo ya China yatatoa fursa nyingi mpya kwa eneo la Asia-Pasifiki na dunia nzima, akiongeza kuwa China inakaribisha pande zote kuendelea kupanda “treni ya mwendokasi” ya maendeleo ya China, kusonga mbele pamoja na China na kufanya juhudi pamoja na China kwenye safari ya nchi zote duniani kujenga mambo ya kisasa ya maendeleo yenye maendeleo ya amani, ushirikiano wa kunufaishana na ustawi wa pamoja.

Kwenye mkutano huo, Rais Xi pia ametangaza kuwa China itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa APEC wa 2026.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha