超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Rais Xi Jinping wa China akutana na mwenzake wa Marekani Joe Biden

(CRI Online) Novemba 18, 2024

(Picha inatoka CRI)

(Picha inatoka tovuti ya CRI)

Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Marekani Joe Biden siku ya Jumamosi kando ya Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia Pasifiki (APEC) mjini Lima, Peru.

Rais Xi amesema kuwa uhusiano kati ya China na Marekani umepitia kipindi cha misukosuko, lakini chini ya uongozi wa pamoja wa marais hao wawili, pande hizo mbili pia zimekuwa zikifanya mazungumzo na ushirikiano wenye ufanisi na kwa ujumla uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelea kwa utulivu.

Amesema kuwa historia ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani imethibitisha uzoefu halisi tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kidiplomasia miaka 45 iliyopita.

Amesema, kama nchi hizo zikiwa washirika na marafiki, zikielewana na kuungana mkono licha ya uwepo wa tofauti, uhusiano wao unaweza kuendelezwa vyema lakini iwapo zitachukuliana kama wapinzani au maadui, zikishindana vibaya na kuumizana, uhusiano wao utaharibiwa na hata kurudishwa nyuma.

Rais Xi amebainisha kuwa binadamu wanakabiliwa na changamoto zisizo na kifani katika dunia ya leo inayokumbwa na misukosuko na migogoro ya mara kwa mara ambapo matatizo ya zamani yanachangiwa na mapya.

Amesema, ushindani kati ya nchi kubwa haupaswi kuwa mantiki ya zama za sasa, ila ni kupitia mshikamano na ushirikiano tu, ndipo zitaweza kutatua changamoto zinazozikabili.

Amesema kuwa, wakati awamu mpya ya mapinduzi ya kisayansi na mageuzi ya kiviwanda inapoendelea, kukatika kwa uhusiano au kuvurugika kwa mnyororo wa ugavi si suluhisho; bali ushirikiano wa kunufaishana ndiyo njia ya kutafuta maendeleo ya pamoja.

Amesema dhana ya "Yadi Ndogo na Uzio Mrefu" siyo suluhisho, bali ni kupitia ushirikiano wa kunufaishana, ndipo pande zote zitaweza kukua pamoja, na kunufaisha binadamu wote.

Amesema, China na Marekani zikiwa nchi kubwa duniani, zinapaswa kuzingatia maslahi ya binadamu wote na kuingiza nguvu chanya zenye uhakika katika dunia ya leo iliyojaa sintofahamu.

Rais Xi amesisitiza kwamba nchi hizo mbili zinapaswa kuzingatia ustawi wa watu wao na maslahi ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa, kufanya maamuzi kwa hekima, kuendelea kutafuta njia sahihi ya nchi hizo mbili kuishi pamoja kwa amani.

Rais Xi amesisitiza kuwa lengo la China la kuhimiza uhusiano tulivu na endelevu na Marekani halijabadilika, kanuni ya China ya kushughulikia uhusiano huo kwa kuheshimiana, kupatana, kushirikiana na kunufaishana haijabadilika, msimamo wa China wa kulinda kithabiti mamlaka, usalama, maslahi ya maendeleo ya taifa haujababilika na matarajio yake ya kuendeleza urafiki wa jadi kati ya watu wa China na Marekani pia hayajabadilika.

Amesema, China inapenda kudumisha mazungumzo, kupanua ushirikiano na kudhibiti tofauti na serikali ya Marekani, na kujitahidi kukipita kwa utulivu kipindi cha mpito cha uhusiano wa China na Marekani, ili kunufaisha watu wa nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha