Lugha Nyingine
Xi Jinping atoa pongezi kwa njia ya video kwa ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Baraza la Mtandao wa Intaneti la Dunia 2024
Tarehe 20, Novemba, rais Xi Jinping wa China akitoa pongezi kwa njia ya video kwa ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Baraza la Mtandao wa Intaneti la Dunia 2024. (Picha/Xie Huanchi)
Tarehe 20, Novemba, rais Xi Jinping wa China alitoa pongezi kwa njia ya video kwa ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Baraza la Mtandao wa Intaneti la Dunia 2024.
Xi Jinping alisema, hivi sasa raundi mpya ya mapinduzi ya teknolojia na mageuzi ya viwanda yanaendelea kwa kasi sana, na teknolojia mpya kama vile akili bandia zinakua siku hadi siku. Teknolojia hizo zimeongeza sana uwezo wa binadamu wa kuijua dunia na kubadilisha dunia, huku zikileta changamoto mbalimbali ambazo ni vigumu kukadiriwa. Tunapaswa kufuata vizuri mwelekeo mkuu wa maendeleo ya kidijitali, maendeleo ya mtandao wa intaneti na maendeleo ya teknolojia ya akili bandia, kuhimiza kwa haraka maendeleo ya uvumbuzi, maendeleo ya usalama na maendeleo ya kuleta manufaa kwa wote wa nafasi ya mtandao wa intaneti, na kushirikiana kupiga hatua kwa kuelekea siku nzuri zaidi za baadaye za “mustakabali wa kidijitali”. China ingependa kushirikiana na nchi mbalimbali duniani, kujenga pamoja jumuiya ya mtandao wa intaneti yenye mustakabali wa pamoja, ili mtandao wa intaneti ulete manufaa mazuri zaidi kwa watu na dunia.
Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Baraza la Mtandao wa Intaneti la Dunia 2024 ulifunguliwa siku hiyo huko Wuzhen, Mji wa Tongxiang wa Mkoa wa Zhejiang wa China, mkutano huo uliandaliwa na Baraza la Mtandao wa Intaneti la Dunia na kuendeshwa na serikali ya Mkoa wa Zhejiang.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma