Lugha Nyingine
Wanadiplomasia wa nchi za Kiarabu watembelea Fujian, Kusini Mashariki mwa China
Mabalozi na wanadiplomasia wa nchi za kiarabu nchini China wakitembelea Jumba la Makumbusho ya Mambo ya Bahari la Quanzhou mjini Quanzhou, Mkoa wa Fujian, kusini-mashariki mwa China, Desemba 1, 2024. (Xinhua/Wei Peiquan)
Hivi karibuni mabalozi na wanadiplomasia 19 wa nchi za kiarabu nchini China walitembelea Mkoa wa Fujian. Ukiwa Mkoa wa Fujian uko kwenye sehemu ya mwisho ya mashariki ya Njia ya Hariri ya Baharini, mkoa huo umetumia nguvu zake bora za kipekee katika utekelezaji wa pamoja wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) na kupata matokeo mengi mazuri katika ujenzi wa eneo la kiini la Njia ya Hariri ya Baharini ya Karne ya 21.?
Mabalozi na wanadiplomasia wa nchi za kiarabu nchini China wakifahamishwa mbinu za utengenezaji wa vinyago vya uso , ambazo ni urithi wa utamaduni usioshikika wa kienyeji, katika jumba la makumbusho ya urithi wa utamaduni usioshikika la Quanzhou, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China, Desemba 1, 2024. (Xinhua/Wei Peiquan)
Mabalozi na wanadiplomasia wa nchi za kiarabu nchini China wakiwa wamepanda basi la kujiendesha katika kampuni ya King Long United Automotive Industry ya Xiamen mjini Xiamen, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China, Novemba 30, 2024. (Xinhua/Wei Peiquan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma