Lugha Nyingine
Taasisi za kigeni zaonesha imani yao kwa uchumi wa China kutokana na utekelezaji wa sera ungaji mkono
Picha iliyopigwa tarehe 10 Januari 2023 ikionyesha mandhari ya eneo la Lujiazui katika Eneo la Majaribio la Biashara Huria la China (Shanghai) mjini Shanghai, mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe)
BEIJING - Benki za kigeni zinazidi kuonyesha imani yao inayoongezeka kuhusu soko la China, ikizingatiwa kwamba sera mbalimbali zilizotekelezwa na serikali ya China tangu mwishoni mwa Septemba, na sera nyingine za awali zinazolenga kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, zimeanza kuleta matokeo endelevu na chanya.
Bill Winters, mtendaji mkuu wa Kundi la Benki za Standard Chartered, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba hatua hizo za sera zilizotolewa na serikali ya China zimekuwa na ufanisi mkubwa katika kupunguza gharama za mambo ya kifedha, hasa katika sekta ya nyumba, wakati mipango hiyo pia inatoa ishara kwamba viongozi wa China wana mpango wa kuchukua hatua kama kuna dalili zozote za wasiwasi.
"Hatua hizo za sera zimekuwa na athari inayotarajiwa ya kubadilisha mwelekeo wa hisia, kote ndani ya wanunuzi na wawekezaji nchini China," Winters amesema.
Wanauchumi na wachambuzi wanaamini kuwa sera hizo zitakuwa na athari kubwa na za muda mrefu kwa uchumi wa China.
"Tunatarajia hatua hizo madhubuti za sera zilizochukuliwa tangu Septemba, kuanzia kupunguzwa kwa viwango vya riba hadi matumizi ya umma, zitasaidia uchumi wa China kudumisha ukuaji wa asilimia 5 Mwaka 2024," amesema Ji Mo, mwanauchumi mkuu wa China wa Kundi la Utafiti la DBS, akiongeza kuwa watunga sera wa China wanajikita katika pande zote mbili kwa muda mfupi na kutoa misingi ya ukuaji endelevu wa muda mrefu.
Kwa kuwa na imani zaidi na uchumi wa China, taasisi nyingi za kigeni zimerekebisha makadirio yao ya ukuaji wa uchumi wa China 2024 kwenda juu.
Kwa mfano, UBS imepandisha makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China mwaka 2024 hadi asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.6, huku Goldman Sachs akipandisha makadirio yake ya ukuaji wa Pato la Taifa la China mwaka huu kutoka asilimia 4.7 hadi asilimia 4.9.
Ufanisi wa hatua hizo za sera ziko wazi nchini China -- huku ufanisi mzuri ukiwa umepatikana katika matumizi kwenye manunuzi, uzalishaji na mauzo ya nyumba, vilevile kasi ya ukuaji wa mauzo ya nje na biashara ya hisa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma