Lugha Nyingine
Maadhimisho ya miaka 25 tangu Macao kurudi China: Watu wa kimataifa wanaoishi Macao waeleza maoni yao
Picha iliyopigwa Agosti 3, 2024 ikionesha sehemu ya Macao. (Xinhua/Cheong Kam Ka)
Miaka 31 iliyopita, Carlos Alvarez kutoka Ureno, mkurugenzi mtendaji mkuu wa sasa wa Benki ya Kitaifa ya Ng'ambo mjini Macao, alifika Macao kwa ajili ya likizo ya mapumziko. Sasa, amekuwa akifanya kazi Macao kwa miaka 6, na anasema, "urafiki" na "urahisi" ni hisia zake kuu kuhusu Macao.
“Macao ina mazingira rafiki ya kijamii na ni moja ya miji salama zaidi duniani. Unaweza kwa urahisi kupata mikahawa yenye ladha (ya vyakula) kutoka duniani kote, na mikahawa ya Michelin yenye bei nafuu hapa.” Alvarez amesema, akiamini kuwa maisha yake yenye wepesi na tulivu ni kutokana na muuunganiko na kukutana kwa tamaduni za Magharibi na Mashariki kulikoletwa na historia ya kipekee ya zamani ya Macao.
Mwaka 2023, Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao wa China ulianzisha mkakati wa maendeleo ya kiuchumi wa “1+4”, unaojumuisha tasnia muhimu kama vile utalii wa mapumziko, afya ya umma, mambo ya kisasa ya fedha, teknolojia ya hali ya juu, maonyesho na biashara, na utamaduni na michezo, ili kuhimiza maendeleo endelevu na yenye ubora wa juu ya uchumi wa Macao.
Kama mtaalamu wa nyanja ya mambo ya fedha, Alvarez anatilia maanani sana sera hiyo. Amesema mkakati huo utasaidia Macao kuvutia kampuni zaidi za kimataifa kuwekeza na kuweka mitaji, kutoa fursa zaidi za ajira, na itanufaisha zaidi maisha ya wakazi wa Macao.
Joao Simons , profesa msaidizi katika Taasisi ya Nchi zinazozungumza Lugha ya Kireno katika Chuo Kikuu cha Mji wa Macao, akifanya kazi ofisini, Novemba 21, 2024. (Picha na Wang Lu/ Xinhua)
Joao Simons, pia kutoka Ureno, ni profesa msaidizi katika Taasisi ya Nchi zinazozungumza Lugha ya Kireno katika Chuo Kikuu cha Mji wa Macao. Amekuwa akiishi hapa kwa miaka 12. Mwaka 2007, Joao, ambaye muda huo alikuwa punde tu amehitimu kutoka chuo kikuu, alitumwa Macao kwa mafunzo ya vitendo kazini na kampuni yake, ingawa alidumu chini ya mwaka mmoja, haraka sana alianza kuipenda Macao.
Miaka miwili baadaye, Joao alirudi China na kusoma Kichina katika miji ya Beijing na Wuhan. Mwaka 2012, Joao, akiwa na umri wa miaka 30 aliacha kazi yake kama mwalimu wa lugha ya kigeni mjini Xian na kurudi Macao pamoja na mke wake. Amesema: "Macao ni ya kipekee sana. Usanifu wa majengo, chakula, lugha na marafiki hapa vyote hunifanya nihisi niko nyumbani."
Kuanzia Julai 10, mwaka huu, Idara ya Kitaifa ya Usimamizi wa Uhamiaji ya China ilianza kutoa Kibali cha Kusafiri kuingia China Bara kwa wakazi wa kudumu wa Macao wasio Wachina, ambacho kina uhalali wa kutumika kwa muda wa miaka mitano. Wakati wa kipindi chote hicho, wanaweza kuingia China Bara mara nyingi, na kila kipindi kimoja cha kuwepo China Bara hakizidi siku 90.
Sera hiyo mpya inahamasisha na kufanya kuwa rahisi kwa wakazi hao kuwekeza, kutembelea ndugu, kusafiri, kufanya biashara, kufanya semina na mabadilishano katika China Bara, hivyo kuhimiza zaidi mabadilishano kati ya watu, ya kiuchumi na kibiashara na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote kwa watu wa pande zote mbili.
Joao ni mmoja wa wanufaika na mpango huo. "Mwaka 2012 tulinunua nyumba Zhuhai, na tukatumia saa mbili au tatu kupanga foleni bandarini ili kusafiri kwenda na kurudi Macao. Sasa kwa kuwa na kibali hiki kipya, inachukua dakika chache tu kuvuka mpaka kwa urahisi," amesema.
Katika miaka ya hivi karibuni, uchumi wa Macao umekuwa shwari na ukiboreka. Idadi kubwa zaidi ya watu wa kigeni wana matumaini kuhusu uwezo na fursa za Macao. Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa hadi kufikia mwisho wa 2023, idadi ya jumla ya waajiriwa wa kigeni mjini Macao ilikuwa imezidi 175,000, ongezeko la zaidi ya 20,000 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma