Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping apokea hati za utambulisho za mabalozi wapya nchini China
Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba baada ya kupokea nyaraka za utambulisho za mabalozi 28 wapya nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Dec. 12, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amepokea nyaraka za utambulisho za mabalozi 28 wapya wa nchi mbalimbali nchini China wakiwemo wa kutoka nchi za Afrika za Mali, Zimbabwe, Chad, Morocco na Somalia jana Alhamisi mjini Beijing.
Akiwakaribisha mabalozi hao Rais Xi amewaomba wafikishe salamu za kutakia kila la kheri kwa viongozi na watu wa nchi zao, akisema kuwa serikali ya China itatoa urahisi na uungaji mkono kwa mabalozi hao katika kutekeleza majukumu yao.
"China ina historia ndefu na eneo kubwa. Natumai mtatembelea maeneo mengi na kusikiliza maoni ya watu wa China ili kuelewa historia ya China, ya sasa na ya siku za baadaye, kujua hali halisi ya China ya leo, njia yake ya maendeleo na mwelekeo wa kusonga mbele," Rais Xi amesema.
Ametoa wito kwa wajumbe hao kujenga madaraja ya mawasiliano, kuhimiza mwelekeo wa ushirikiano, na kuenzi urafiki kati ya China na nchi zao na nchi nyingine mbalimbali.
Rais Xi amesema, "Ujenzi wa mambo ya kisasa wa China hauhusu China kufanya vema peke yake," China inapenda kuchangia fursa zake za maendeleo na nchi nyingine na kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa wa nchi mbalimbali kwa ajili ya kutimiza maendeleo ya amani, ushirikiano wa kunufaishana na ustawi kwa pamoja.
Wakati dunia inakabiliwa na changamoto na misukosuko mikubwa, kama vile hali ya migogoro ya siasa za kijiografia inayozidi kuwa mbaya, hatua za upande mmoja, kujilinda kiuchumi, na mabadiliko ya tabianchi, ni muhimu kwamba nchi zote zichukue hatua za pamoja, amesema.
Rais Xi amesisitiza kuwa China inashikilia kufuata njia ya maendeleo ya amani, China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali katika kutetea Dunia ya ncha nyingi yenye usawa na utaratibu na utandawazi wa kiuchumi wenye manufaa na jumuishi kwa wote, ili kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.?
Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba baada ya kupokea nyaraka za utambulisho za mabalozi 28 wapya nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Dec. 12, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)
Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba baada ya kupokea nyaraka za utambulisho za mabalozi 28 wapya nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Dec. 12, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma