超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Kuwalewa tena "wanunuzi wa China"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 13, 2024

Je, umebadilika katika suala la manunuzi?

Katika miaka ya hivi karibuni, mahitaji ya manunuzi na dhana za manunuzi za watu vinabadilika. Katika muktadha wa kuhamasisha kwa nguvu manunuzi, ni muhimu sana kuwaelewa tena "wanunuzi wa China".

Je, wanunuzi wa China ni "wahafidhina"?

Kwa muda mrefu, dhana ya "kihafidhina" ya jadi ya China na mawazo ya manunuzi vinaonekana kuwa vimetengeneza kasumba. Je, bado ni hivyo leo? Hebu tutazame seti hizi mbili za takwimu:

Mwezi Novemba mwaka huu, soko la China la magari ya abiria liliuza magari milioni 2.423, ambapo magari yanayotumia nishati mpya yaliyouzwa yalikuwa milioni 1.268, yakiwa na kiwango cha kupenya cha 52.3%, yakipita magari yanayotumia mafuta kwa mwezi wa tano mfululizo. Magari yanayotumia nishati mpya ya China yanaweza kuongoza dunia leo, kwa kiasi fulani, na wanunuzi wa China "wameyanunua" kwa pesa halisi! Utayari wa kukubali mambo mapya umekuwa sifa mpya ya wanunuzi wa China.

Je, wanunuzi wa China "wanaabudu vitu vya kigeni"?

Siku za nyuma, bidhaa za maziwa za Australia na vifaa vidogo vya Japan vilitafutwa sana na watu wa China; sasa, sketi zenye uso wa farasi, vinywaji vipya vya chai ya Kichina, na "Black Myth: Wukong" vimekuwa "mtindo maarufu" mpya wa China na mara kwa mara "mashabiki wa mzunguko" nje ya nchi.

Ushawishi wa utamaduni wa jadi juu ya mwenendo wa manunuzi unaendelea kuongezeka. Mwezi Mei mwaka huu, wiki moja baada ya matangazo ya mtandaoni ya "My Altay ", umaarufu wa utafutaji wa neno "Altay" kwenye mtandao wa safari wa Tongcheng uliongezeka kwa 562%. Mwezi Agosti, mchezo wa kompyuta uliobuniwa China wa "Black Myth: Wukong" uliendelea kuwa maarufu nchini China na "kuvutia mashabiki" nje ya nchi.

Ikiwa ni mandhari kuu ya kurekodi maudhui ya mchezo huo, ufuatiliaji wa mada ya utamaduni na utalii wa Shanxi uliongoza kwenye orodha, ukipata ukuaji maradufu katika mapokezi na mapato ya utalii. Wanunuzi wa China wanakuwa na imani zaidi na zaidi katika utamaduni wao wenyewe!

Je wanunuzi wa China "wamefungwa"?

Chakula kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) hubeba mila na urithi wa kitamaduni duniani kote, biashara ya mtandaoni ya kuvuka mipaka ambayo imekuwa sehemu mpya ya ukuaji katika kipindi cha "Double 11" (Ghulio la Manunuzi Mtandaoni la Novemba 11 kila mwaka), na kuendelea kuongezeka kwa umaarufu wa watalii wa China kwenda ng'ambo….Wanunuzi wa China wanaikumbatia dunia kwa mtazamo jumuishi na wa wazi, wakivutia kampuni za kimataifa kuingia China na kuzalisha bidhaa zaidi zinazokidhi matakwa ya wanunuzi wa China.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, wakuu wa kimataifa wa kampuni kadhaa za kimataifa kama vile Apple, Qualcomm, Mercedes-Benz, na Tesla wametembelea China kwa wingi. Hii siyo tu kura ya kuwa na imani katika fursa za sera za China, lakini pia kura ya kuwa na imani katika wanunuzi wa China.

Je, wanunuzi wa China "ni wenye hulka ya kibinafsi"?

Wanunuzi wa China, ambao hapo awali walijulikana kwa asili yao ya "kujizuia na kujiweka pembeni", sasa wana "shauku kubwa ya kuchangia maudhui" kwenye mitandao ya kijamii.

Ripoti za umma zinaonyesha kuwa idadi ya sasa ya kila mwezi ya akaunti za WeChat zinazotumika imefikia bilioni 1.382; kwenye mtandao wa Kichina wa Xiaohongshu, idadi hiyo ya watumiaji wanaoutumia kila mwezi imezidi milioni 300.

Kwa sasa, "wanunuzi wa China" wanahitaji kutambuliwa tena: wako tayari kukubali mambo mapya, kutoa fursa za uvumbuzi; wamejaa imani na wanaunga mkono bidhaa za mtindo mpya za China; wana upeo mpana na hupokea nguo na bidhaa za kimataifa; wanapenda kuchangia na wengine na kusaidia kunadi bidhaa nzuri ili ziwe maarufu duniani kote. Kiwango hicho hakina kifani, ubora ni wa juu, na uvumbuzi unazidi kuongezeka. Hili ndilo soko la China!

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha