Katika miaka ya hivi karibuni, magari mengi zaidi na zaidi yanayotumia nishati mpya yaliyozalishwa mkoani Hubei, China yamesafirishwa kuuzwa nchi za nje kupitia treni ya China-Ulaya (Wuhan). Bei ya usafirishaji huo ni sehemu ya moja ya tano ya usafirishaji wa anga, na mtandao wa huduma yake unafika karibu bara zima la Asia-Ulaya, Eurasia.
Hapa koili ya chuma cha pua inaweza kuzalishwa kila baada ya sekunde 90, tanuri la kuyeyusha chuma cha pua hujazwa kila baada ya dakika 30, na koili za chuma cha pua za tani 1,200 zinaweza kuzalishwa ndani ya saa moja. Kiwanda hicho kinatumia teknolojia zaidi ya 130 za uzalishaji wa kijani wa chuma cha pua, kikiweza kutumia kwa asilimia 100 mabaki ya uzalishaji wa chuma cha pua.
Siku ya Jumapili, Mei 26, usiku ulipoingia, mara hali motomoto imeonekana kwenye Mtaa wa Utamaduni na Ubunifu ya Taoxichuan mjini Jingdezhen, Mkoa wa Jiangxi wa China taratibu. Kiwanda cha zamani cha vyombo vya kauri kilichotelekezwa sasa kimekuwa alama ya kitamaduni ya mji huo.
Siku ya tano ya mwezi wa tano kwa kalenda ya kilimo ya China ni Sikukuu ya jadi ya Duanwu ya China, pia inajulikana ni siku ya mashindano ya mashua ya Dragoni, wakati sikukuu hiyo inapokaribia, watalii wanaotembea na kusimama kwenye barabara za Mtaa wa Kale wa Yuehe huko Jiaxing wakiwa nyuma ya mandhari ya kuta nyeupe na vigae vyeusi huunda picha nzuri ya mandhari ya Jiangnan ambayo ni sehemu ya kusini mwa Mto Changjiang. Mtaa wa Kihistoria wa Jiaxing Yuehe ni mtaa wa kale mkubwa zaidi na wenye mpangilio kamilifu zaidi wa kihistoria katika Mji wa Jiaxing, eneo la mtaa huo lina mita za mraba 90,000, ambapo majengo 29 ya kihistoria yamehifadhiwa vizuri mtaani.