Lugha Nyingine
Rais Xi ahimiza hatua kali zaidi ili kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi kwa pamoja
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China Jumatatu wiki hii ametoa wito kwa pande zote kuchukua hatua madhubuti ili kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa pamoja.
Xi ameyasema hayo katika hotuba yake ya maandishi kwa ajili ya Mkutano wa Viongozi wa Dunia katika kikao cha 26 cha Mkutano wa Nchi Wanachama (COP26) kuhusu Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya hali ya hewa, unaofanyika mjini Glasgow kuanzia Jumatatu hadi Jumanne.
"Natumai pande zote zitachukua hatua kali zaidi kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi kwa pamoja na kulinda sayari ya dunia, nyumba ya pamoja kwa ajili yetu sote." amesema.
Athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa zimezidi kudhihirika, na kuleta uharaka unaoongezeka wa hatua za kimataifa, amesema.
Rais huyo wa China ametoa mapendekezo matatu kushughulikia changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono makubaliano ya pande nyingi, kuzingatia hatua madhubuti, na kuharakisha mabadiliko ya kijani kibichi.
"Linapokuja suala la changamoto za kimataifa kama vile mabadiliko ya hali ya hewa , ushirikiano wa pande nyingi ni dawa sahihi." amesema.
Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya hali ya hewa na Makubaliano ya Paris ya mwaka 2015 yametoa msingi wa kisheria wa ushirikiano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Pande husika zinahitaji kujenga juu ya makubaliano yaliyopo, kuongeza kuaminiana, kuongeza ushirikiano na kufanya kazi pamoja ili kuufanya mkutano wa COP26 wenye mafanikio huko Glasgow, ameongeza.
Pande husika zinahitaji kuheshimu ahadi zao, kuweka malengo na maono ya kweli, na kufanya kila linalowezekana kulingana na hali halisi ya nchi ili kutoa hatua za utekelezaji za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, Xi amesema.
Rais wa China amesisitiza wajibu wa nchi zilizoendelea katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, akisema kwamba hazipaswi kufanya zaidi kwa upande wake zenyewe, bali pia zinapaswa kutoa msaada ili kuzisaidia nchi zinazoendelea kufanya vizuri zaidi.
Hivi karibuni China imetoa mpango wa utekelezaji wa kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni kabla ya Mwaka 2030, pamoja na waraka wenye jina la "Mwongozo Kazi wa Kupunguza utoaji wa hewa ya Kaboni na Kufikia uwiano wa Kaboni Katika Utekelezaji Kamili na Uaminifu wa Wazo jipya la kujipatia Maendeleo."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma