Lugha Nyingine
Mapacha wa simba wachanga walioachwa na mama yao wakua vizuri
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 15, 2022
Picha ikionesha mmoja wa mapacha wa simba wachanga wa Afrika huko Chongqing, China. (ChinaDaily/Wang Chengjie) |
Mapacha wa simba wachanga wa Afrika walioachwa na mama yao punde tu baada ya kuzaliwa kwao, hivi sasa wana hali nzuri ya afya.
Mapacha hawa wa kike wanaoitwa na watu kuwa “Rourou” na “Tuantuan” walizaliwa kwenye Bustani ya Lejia ya Chongqing mwezi uliopita. Mama yao ni simba mzee, ambaye alikataa kuwalea watoto wake. Mapacha hao wenye njaa walipelekwa kwenye kituo cha uokoaji, kuzaliana na kutunza cha bustani na kulewa na wafanyakazi huko.
Mhuduma Chen Wei alisema, uzito wa wachanga umezidi kwa maradufu, ukiongezeka kutoka kilogramu 3 hadi 6.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma