超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Simulizi ya Zawadi za Kitaifa za Rais Xi: Treni ya Mwendokasi ya "Fuxing" modeli ya EMU

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 20, 2023
Simulizi ya Zawadi za Kitaifa za Rais Xi: Treni ya Mwendokasi ya
Mfano wa Treni ya Mwendokasi ya "Fuxing" modeli ya EMU aliyopewa Waziri Mkuu wa Thailand Prayut Chan-o-cha na Rais Xi Jinping wa China. (Chanzo: CCTV)

Kuanzia Novemba 17 hadi 19, 2022, Rais Xi Jinping wa China alihudhuria kwenye Mkutano wa Viongozi wa Nchi wanachama wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Nchi za Asia Pasifiki (APEC) huko Bangkok, Thailand na kufanya ziara nchini Thailand. Na alitoa zawadi ya kitaifa kwa upande wa Thailand - Treni ya Mwendokasi ya "Fuxing" modeli ya EMU.

Tofauti na treni za kawaida za mwendo kasi nchini China, rangi ya mfano wa treni hiyo ya mwendokasi modeli ya EMU ni sawa na rangi za Bendera ya Taifa ya Thailand. Na treni hiyo halisi ya kawaida ya China itaendeshwa kwenye njia ya Reli ya China-Thailand.

Ukiwa ni mradi mkuu wa pamoja wa China na Thailand wa ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na ujenzi wa reli ya kwanza ya mwendo kasi ya SGR nchini Thailand, Reli ya China-Thailand inatumia teknolojia ya EMU ya "Fuxing" kwa kufuata vigezo vya China.

Mafungamano ya mawasiliano kati ya nchi hizo mbili pia yataleta manufaa kwa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta za uchumi, biashara na utamaduni. Mwaka 2021, thamani ya jumla ya biashara kati ya China na Thailand ilizidi dola bilioni 100 kwa mara ya kwanza, na kufikia dola za Kimarekani bilioni 131.2, ikiwa ni ongezeko la 33% kuliko ile ya mwaka 2020.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha