超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Simulizi za Zawadi za Kitaifa za Rais Xi: Matoleo 19 ya People's Daily

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 26, 2023
Simulizi za Zawadi za Kitaifa za Rais Xi: Matoleo 19 ya People's Daily
Picha hii ikionyesha ukurasa wa kwanza wa Gazeti la People's Daily toleo la Juni 26, 1955.

Novemba 13, 2017, mbele ya nyumba ya zamani ya Ho Chi Minh aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam, Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China alitoa zawadi ya matoleo 19 ya Gazeti la People's Daily kwa Nguyen Phu Trong, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam.

Kati ya magazeti hayo, magazeti ya matoleo matatu yalichapisha habari kuhusu ziara ya Nguyen Phu Trong nchini China mnamo Januari, 2017. Kuhusu magazeti ya matoleo mengine 16, Rais Xi aliyajulisha kwa kusema:"Hayo ni magazeti yaliyochapisha habari za ziara ya Rais Ho Chi Minh nchini China Mwaka 1955, na tumeyapata kwa jitihada." Rais Nguyen Phu Trong alishangaa na kufurahi sana baada ya kusikia hayo.

Ukurasa wa kwanza wa Gazeti la People's Daily toleo la Juni 26, 1955 ilikuwa ni picha ya Mao Zedong, Zhou Enlai na viongozi wengine waanzilishi wa Chama cha Kikomunisti cha China wakiwa pamoja na Ho Chi Minh. Siku iliyofuata, pia katika ukurasa wa mbele wa Gazeti la People's Daily, hotuba ya Ho Chi Minh ilichapishwa:"Hakuna shaka kwamba urafiki na uhusiano wa karibu kati ya watu wa China na Vietnam ni wa milele na usiovunjika, pia hauwezi kutenganishwa au kuzuiliwa na mtu yeyote."

Novemba 13, 2017, Rais Xi Jinping na Rais Nguyen Phu Trong walizungumza huku wakitembea kwenye nyumba ya zamani ya Ho Chi Minh. Rais Xi alisema:"Tunapaswa kujifunza kutoka kwa Mwenyekiti Mao, Waziri Mkuu Zhou na Rais Ho Chi Minh, na kuupeleka mbele na kuuendeleza uhusiano wa kirafiki wa China na Vietnam ili kunufaisha zaidi watu wa nchi zetu mbili."

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha