Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping akagua Mji wa Shaoxing katika Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 22, 2023
HANGZHOU - Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amekagua Mji wa Shaoxing wa Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa wa China siku ya Jumatano alasiri.
Rais Xi ametembelea ukumbi wa maonyesho kuhusu “Uzoefu wa Fengqiao" akifahamishwa mchakato wa kutolewa na kuendelea kwa uzoefu wa Fengqiao kuhusu usimamizi wa jamii mashinani, na hali yake ya uvumbuzi na maendeleo katika zama mpya.
Pia ametembelea bustani ya utamaduni wa mfereji ili kufahamishwa kuhusu historia ya mfereji wa kale, uhifadhi wa Mfereji Mkuu, na hali ya ujenzi wa bustani ya utamaduni ya kitaifa ya Mfereji Mkuu.?
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma