Lugha Nyingine
Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Vietnam Vo Van Thuong
Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Xi Jinping amefanya mazungumzo na Rais wa Vietnam Vo Van Thuong kwenye Ikulu ya Hanoi, Vietnam asubuhi ya tarehe 13, Desemba kwa saa za Vietnam.
Kwenye mazungumzo hayo, Rais Xi Jinping amesema, kujenga jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja ambayo ina umuhimu wa kimkakati kunaendana na maslahi ya pamoja ya watu wa nchi hizo mbili. Na kwamba, pande hizo zinatakiwa kuimarisha mwongozo wa kisiasa, kuimarisha mshikamano na uratibu, kuongeza ushirikiano wa kunufaishana, kuongeza mwongozo wa maoni ya umma, na kushughulikia tofauti ipasavyo.
Kwa upande wake Vo Van Thuong amesema, uhusiano wa Vietnam na China haujawahi kuwa kamilifu, wa kina na wa kirafiki kama ulivyo sasa. Amesema, kuendeleza uhusinao na China siku zote kumekuwa kipaumbele cha juu na chaguo la kimkakati la chama na serikali ya Vietnam.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma