Lugha Nyingine
Bustani ya Theluji na Barafu?ya Harbin, China yafunguliwa kwa umma
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 19, 2023
Picha hii ikionyesha eneo la Bustani ya Barafu na Theluji ya Harbin mjini Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, Kaskazini-Mashariki mwa China, Desemba 18, 2023. (Xinhua/Xie Jianfei) |
Bustani maarufu duniani ya Barafu na Theluji ya Harbin imefunguliwa rasmi kwa umma siku ya Jumatatu mjini Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, Kaskazini-Mashariki mwa China. Mandhari na sanamu za kuvutia za barafu na theluji zaidi ya 1,000 zimejengwa katika bustani hiyo ili kuwapa burudani na furaha ya kipekee watu wanaotembelea. Bustani hiyo inalenga kuunganisha sanaa, utamaduni, maonyesho ya jukwaani, usanifu majengo na michezo ili kuonyesha haiba nzuri ya barafu na theluji.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma