超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Rais Xi Jinping ampongeza Shehbaz Sharif kwa kuchaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Pakistan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 04, 2024

BEIJING – Siku ya Jumapili iliyopita, Rais wa China Xi Jinping amempongeza Shehbaz Sharif kwa kuchaguliwa kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Pakistan, akisema kuwa anaamini chini ya uongozi wa Sharif na serikali mpya ya Pakistan, na kwa juhudi za pamoja za wananchi wa sekta zote nchini Pakistan, hakika nchi hiyo itapata mafanikio mapya na makubwa zaidi katika mambo ya maendeleo na upigaji hatua wa nchi hiyo .

Rais Xi amesisitiza kuwa China na Pakistan zinapaswa kuendeleza urafiki wao wa jadi, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano katika sekta zote, kujenga kwa pamoja mradi mpya ulioboreshwa wa Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan, kuendelea kuimarisha uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa siku zote kati ya China na Pakistan, na kujenga jumuiya ya karibu ya China na Pakistan yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.

Siku hiyo, Waziri Mkuu wa China Li Qiang pia alituma salamu za pongezi kwa Sharif.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha