Lugha Nyingine
Mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China wafunguliwa
Kikao cha ufunguzi wa mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 5, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
BEIJING – Mkutano wa Pili wa Bunge la Umma la 14 la China umefunguliwa leo siku ya Jumanne asubuhi kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, ambapo Xi Jinping na viongozi wengine wa China wamehudhuria kikao hicho cha ufunguzi wa mkutano.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang ametoa ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano huo.
Wajumbe wamepitia ripoti hiyo ya Baraza la Serikali la China kuhusu utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii wa Mwaka 2023 pamoja na mswada wa mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii wa Mwaka 2024.
Pia wamepitia ripoti ya Baraza la Serikali la China kuhusu utekelezaji wa bajeti ya serikali kuu na ya serikali za mitaa ya Mwaka 2023 pamoja na mswada wa bajeti ya serikali kuu na ya serikali za mitaa ya Mwaka 2024.
Li Hongzhong, naibu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, ameelezea mswada wa marekebisho wa Sheria ya kimsingi kuhusu utaratibu wa muundo wa vyombo na utaratibu wa kazi wa Baraza la Serikali la China kwenye kikao hicho cha ufunguzi wa mkutano.?
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akitoa ripoti ya kazi ya serikali kwenye kikao cha ufunguzi wa mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 5, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)
Zhao Leji akiongoza kikao cha ufunguzi wa mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 5, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)
Li Hongzhong, naibu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China akifafanua mswada wa marekebisho ya Sheria ya kimsingi kuhusu utaratibu wa muundo wa vyombo na utaratibu wa kazi wa Baraza la Serikali la China katika kikao cha ufunguzi wa mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 5, 2024. (Xinhua/Liu Weibing)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma