Lugha Nyingine
Viongozi waandamizi wa China wajumuika na Wajumbe wa Bunge la Umma la China, washauri wa kisiasa katika majadialino na mashauriano
Li Qiang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Waziri Mkuu wa China akishiriki katika majadiliano na wajumbe wa ujumbe wa Mkoa wa Guangdong kwenye mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China mjini Beijing, Machi 6, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)
BEIJING - Viongozi waandamizi wa China Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi Jumatano walihudhuria mijadala kwenye mkutano wa pili cha Bunge la Umma la 14 la China na majadiliano ya vikundi kwenye mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC).
Li Qiang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Waziri Mkuu wa China, ameuhimiza Mkoa wa Guangdong uwe mtangulizi katika kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa ya China, wakati alipojumuika na wajumbe wa Bunge la Umma la China kutoka mkoa huo kwa majadiliano.
Ameutaka mkoa huo kuendeleza mageuzi na ufunguaji mlango kwa dhamira kubwa na juhudi kubwa zaidi, kuendeleza maendeleo yaliyoratibiwa kati ya mikoa na kati ya maeneo, na kati ya miji na vijiji, kuboresha maisha ya watu, na kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu.
Wakati alipojumuika na washauri wa kisiasa kutoka sekta ya uchumi na kilimo, Waziri Mkuu Li amesema kuwa China itaendelea kutekeleza kwa juhudi kubwa sera za mambo ya fedha na kufuata sera ya fedha kwa hatua madhubuti mwaka huu.
Wakati akihudhuria mijadala ya washauri wa kisiasa kutoka Chama cha Muungano wa Kidemokrasia cha China na Chama cha Kidemokrasia cha Wakulima na Wafanyakazi wa China, Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la China, ameeleza matumaini yake kuwa washauri hao wa kisiasa watatafuta nafasi yao inayofaa na kudumisha mwelekeo wazi katika mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.
Akiungana na washauri wa kisiasa kutoka makabila madogo, Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa, amewataka washauri hao wa kisiasa watimize wajibu na majukumu yao kikamilifu na kuongeza juhudi katika majadiliano na mashauriano.
Wang amesisitiza kuwa washauri hao wa kisiasa wanatakiwa kutoa mchango kwa ajili ya kujumuisha uelewa wa watu kwenye jamii kwa taifa la China na kuhimiza mshikamano na maendeleo ya kikabila.
Cai Qi, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, alishiriki katika mkutano wa pamoja wa washauri wa kisiasa kutoka sekta za fasihi, sanaa na michezo. Amewataka kuchangia hekima na juhudi katika kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa ya China, na kutoa mchango katika kuijenga China kuwa nchi inayoongoza katika utamaduni na michezo.
Ding Xuexiang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na naibu waziri mkuu wa China, alihudhuria mkutano wa pamoja wa washauri wa kisiasa kutoka mikoa ya utawala maalum ya Hong Kong na Macao.
Ding amesisitiza kuunga mkono Hong Kong katika kukamilisha mchakato wa kutunga sheria ya Kifungu cha 23 cha Sheria ya Msingi ya HKSAR haraka iwezekanavyo, na akisisitiza kukamilisha mifumo na taratibu za kulinda usalama wa taifa huko Macao na kuhakikisha utekelezaji thabiti na endelevu wa “nchi moja, mifumo miwili."
Li Xi, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Ukaguzi wa Nidhamu ya Kamati Kuu ya CPC alihudhuria mkutano wa pamoja wa washauri wa kisiasa kutoka Chama cha kidemokrasia cha Jiusan Society cha China na watu wasio na chama. Amesisitiza kushinda vita vikali na vya muda mrefu dhidi ya ufisadi.?
Li Qiang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Waziri Mkuu wa China akihudhuria kwenye mkutano wa pamoja wa washauri wa kisiasa kutoka sekta za uchumi na kilimo kwenye mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) mjini Beijing, Machi 6, 2024. (Xinhua/Rao Aimin)
Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Umma la China, akihudhuria kwenye mkutano wa pamoja wa washauri wa kisiasa kutoka Chama cha Muungano wa Kidemokrasia cha China na Chama cha Kidemokrasia cha Wakulima na Wafanyakazi cha China kwenye mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) mjini Beijing, Machi 6, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)
Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China, akihudhuria mkutano wa pamoja wa washauri wa kisiasa kutoka makabila madogomadogo ya China kwenye mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) mjini Beijing, Machi 6, 2024. (Xinhua/Shen Hong)
Cai Qi, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya CPC, akihudhuria kwenye mkutano wa pamoja wa washauri wa kisiasa kutoka sekta za fasihi, sanaa na michezo kwenye mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) mjini Beijing, Machi 6, 2024. (Xinhua/Yan Yan)
Ding Xuexiang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu wa China akihudhuria kwenye mkutano wa pamoja wa washauri wa kisiasa kutoka mikoa ya utawala maalum ya China ya Hong Kong na Macao kwenye mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) mjini Beijing, Machi 6, 2024. (Xinhua/Gao Jie)
Li Xi, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Ukaguzi wa Nidhamu ya Kamati Kuu ya CPC akihudhuria kwenye mkutano wa pamoja wa washauri wa kisiasa kutoka Chama cha Kidemokrasia cha Jiusan Society cha China na watu wasio na chama kwenye mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) mjini Beijing, Machi 6, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma