Lugha Nyingine
Msemaji wa jeshi la China ajibu maswali ya waandishi wa habari kwenye mkutno mkuu wa mwaka wa Bunge la Umma la China
BEIJING - Wu Qian, msemaji wa ujumbe wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China na Jeshi la Polisi la China kwenye mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China unaoendelea, siku ya Jumamosi alijibu maswali ya wanahabari na kujibu maswali kuhusu maoni na mapendekezo ya wajumbe wa majeshi hayo kuhusu jeshi, bajeti ya ulinzi ya China, na mauzo ya silaha ya Marekani kwa Taiwan ya China.
Wakati wa majadiliano kwenye mkutano mkuu wa bunge la umma, wajumbe wa ujumbe wa kijeshi wamesema ni lazima kuimarisha ugavi wenye ufanisi kwa ajili ya uwezo wa hali ya juu wa kupigana vita, na kuufanya ulinzi wa taifa la China na vikosi vya jeshi kuwa vya kisasa kutokana na nguvu ya jumla ya nchi ya China, Wu amesema.
Akijibu swali kuhusu bajeti ya ulinzi, Wu amesema matumizi ya ulinzi ya China ni ya wazi, ya halali na yanayofaa.
Ripoti ya bajeti iliyowasilishwa na kujadiliwa kwenye mkutano wa bunge la umma imeonesha kuwa, mwaka huu, China inapanga kutumia yuan trilioni 1.66554 (kama dola za kimarekani bilioni 234.5) kwa ulinzi wa taifa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.2 kutoka takwimu halisi ya mwaka 2023.
China hivi sasa inakabiliwa na hali yenye utatanishi na changamoto katika mapambano dhidi ya mafarakano, huku kukiwa na kazi ngumu za kijeshi na kuzidi kwa hali isiyo ya utulivu na kutokuwa na uhakika katika mazingira ya usalama wa nchi, Wu amesema.
Amesema kiasi kilichoongezeka cha matumizi ya ulinzi kitatumika hasa kuongeza mafunzo ya kijeshi, kuimarisha maandalizi ya kupigana vita, kuharakisha maendeleo ya uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia unaohusiana na ulinzi, na kuimarisha mageuzi ya ulinzi wa taifa na majeshi.
Akijibu swali kuhusu mauzo ya silaha ya hivi karibuni ya Marekani kwa eneo la Taiwan la China, Wu amesema China ingependa kuonesha udhati mkubwa zaidi na kufanya kila iwezalo kwa kujitahidi kufikia muungano wa taifa wa amani.
"Lakini kamwe hatutaacha nafasi yoyote kwa shughuli za makundi yanayojaribu kuifanya 'Taiwan ijitenge,'" ameongeza.
Amesema Taiwan ni Taiwan ya China, na suala la Taiwan ni suala la mambo ya ndani ya China ambalo haliruhusu uingiliaji wa nje.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma