Lugha Nyingine
Video: Simulizi za demokrasia
Katika ardhi kubwa ya China wanaishi watu zaidi ya bilioni 1.4. Wengine wanaeleza kwa dhati maoni kutoka mioyoni mwao. Wengine wanasikiliza kwa umakini.
Hapa kuna mwanamume, mjumbe mwenye ulemavu wa macho wa Bunge la Umma la 14 la China, ambaye pendekezo lake liliwekwa kwenye sheria.
Hapa kuna mwanamke, mzazi aliyeandika ujumbe kwenye Ukurasa wa Ujumbe kwa Viongozi wa tovuti ya People's Daily, ambaye ameshuhudia shule ya mtoto wake ikihamishiwa hadi kwenye jengo jipya.
Hapa, chumba cha upatanishi kinachoitwa "Chumba cha Upatanishi cha Dombra" kinaingiza mila na desturi katika kushughulikia kesi.
Mifano hii yote inathibitisha ukweli kwamba nchini China, demokrasia inashikika, inaonekana, yenye kutegemea watu, na yenye matokeo halisi.
Demokrasia si pambo la kutumika kwa kufanya mapambo; inatumika kwa kutatua matatizo ambayo wananchi wanataka kutatua. Watu ndiyo msingi na lengo la demokrasia ya umma ya mchakato mzima.
Demokrasia ya umma ya mchakato mzima inahakikisha kwamba watu wanaendesha nchi na kuisukuma China kuendelea kupiga hatua za maendeleo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma