Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa wito kwa Chongqing kuandika ukurasa wake wa ujenzi wa mambo ya kisasa ya China
CHONGQING - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) kwenye ziara yake ya ukaguzi katika Mji wa Chongqing, Kusini Magharibi mwa China ametoa wito kwa mji huo kuendeleza kwa kina zaidi mageuzi na ufunguaji mlango kwa pande zote, na kuandika ukurasa wake kwa ajili ya kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.
Chongqing inapaswa kujitahidi kuhimiza maendeleo ya sifa bora, na kujijenga kuwa egemeo kuu la kimkakati kwa maendeleo ya eneo la magharibi la China katika zama mpya na kuwa kituo cha kuunganisha pande zote cha ufunguaji mlango wa eneo la bara, Rais Xi amesema. Wakati akikagua eneo maalum la kituo cha kimataifa cha usafirishaji bidhaa cha Chongqing siku ya Jumatatu alasiri, Rais Xi alisema kuwa sekta ya usambazaji wa bidhaa ndiyo inayounda ateri na mishipa ya uchumi halisi. Amesisitiza kuwa ujenzi wa Ushoroba Mpya wa Biashara ya Kimataifa ya Nchi Kavu na Baharini utasaidia kuhimiza ufunguaji mlango wa kiwango cha juu wa maeneo ya magharibi na bara ya China.
Kisha Rais Xi alitembelea kituo cha kontena, ambapo alisisitiza umuhimu wa sekta ya usafirishaji bidhaa katika kuendesha maendeleo ya eneo la magharibi.
Baada ya kusikiliza ripoti ya ujenzi wa mzunguko wa kiuchumi wa Chengdu-Chongqing, Rais Xi ameitaka Chongqing kujikita katika uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia na kuhamasisha kwa nguvu maendeleo ya sifa bora ya viwanda vya utengenezaji wa bidhaa.
Wakaki akitembelea eneo la nyumba za wakazi zilizojengwa zamani lililofanyiwa ukarabati kuanzia mapema mwaka 2022, Rais Xi alifahamishwa juu ya ukarabati na huduma za kijamii katika eneo hilo la makazi, na alizungumza na wakaazi waliokuwa wakila chakula kwenye kantini ya eneo la makazi, akisema ukarabati wa eneo la makazi lililojengwa zamani unapaswa kuhifadhi kumbukumbu za kihistoria na wakati huo huo kutatua matatizo yanayofuatiliwa na wakaazi.
Siku ya Jumatano asubuhi, Rais Xi alisikiliza ripoti za kazi ya kamati ya Chama na Serikali ya Mji wa Chongqing, na kuthibitisha mafanikio ya Chongqing katika pande mbalimbali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma