Lugha Nyingine
Hali ya Maisha mjini Xi’an ni nzuri iliyoje (6)
Katika mtaa wa Soko la Enzi ya Tang la siku nzima,watalii wakichagua sanaa ya mikono. (Weng Qiyu/People’s Daily Online) |
Wakati wa jioni, ukitembelea kwenye Soko la Enzi ya Tang la uwazi wa usiku kucha, unaweza kuona watu wengi wanaovaa mavazi ya kijadi ya China wakipiga picha karibu na ukuta mwekundu. “Nahisi kama nimepita katika wakati wa enzi ya zamani! Nataka kurekodi urembo wangu kwenye hali nzuri ya jioni ya “Mji wa Chang’an (uliokuwa Mji Mkuu wa China katika Enzi ya Tang) ”. alisema Bibi Su, mtalii anayetoka Mji wa Chongqing.
Katika Mtaa wa watu wa Kabila la Wahui, kuna vyakula vya aina mbalimbali, kama vile: nyama ya kuokwa ya Hongliu, Keki ya Maua ya Guihua, Paomo(Mkate laini unaowekwa supuni). Sauti ya watalii ya kununua vyakula na sauti ya kuuza ya wafanyabiashara zimesikika pote bila kusita.
Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Xi’an unalenga kujenga mji unaoonesha dunia ustaarabu wa China, na kufanya juhudi zaidi za kujenga chapa ya mji ya “Karibu Mji wa Chang’an wenye historia ndefu”. Habari zinasema kuwa mwaka 2024, Mji wa Xi’an utatafuta zaidi thamani ya utamaduni wa mji huo, na kufanya juhudi za kupata maendeleo mapya na kuonesha sura mpya ya utamaduni wake mzuri wa kijadi wa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma