Lugha Nyingine
Soko la Ubunifu la Mji wa Jingdezhen katika Mkoa wa Jiangxi, China lawa maarufu
Picha iliyopigwa Mei 26 ikionyesha mazingira ya usiku ya Soko la Ubunifu la Jingdezhen Taoxichuan katika Mkoa wa Jiangxi, China. (Picha na Shi Yu/People's Daily Online) |
Jioni ya Mei 26, Soko la Sanaa za Ubunifu katika Mtaa wa Utamaduni na Ubunifu wa Taoxichuan mjini Jingdezhen, Mkoa wa Jiangxi wa China, lilikuwa limejaa watu. Vibanda vya bidhaa zaidi ya 400 vilikuwa vimepangwa kwa mstari mrefu, na vyombo vya kauri vinavyoonesha ubunifu wa aina mbalimbali vilivutia watalii kusimama na kuchagua.
Kutembea kwenye soko hilo la usiku, inaonekana kama kuwa katika bahari ya kauri. Usanifu na ubunifu wa kisasa wa aina mbalimbali umeingiza nguvu mpya kwenye kauri za kijadi.
Kwa kutegemea utamaduni wa kauri wenye historia ya miaka elfu moja, katika miaka ya hivi karibuni, mjini Jingdezhen kumeanzishwa kwa mtaa wa Taoxichuan na sehemu nyingine za kuwavutia watu wanaojulikana mtandaoni ili kuhimiza mafungamano ya utamaduni na utalii, na kuwezesha hali ya kuhimizana kwa kazi ya ulinzi wa utamaduni wa kauri na maendeleo ya sekta ya utamaduni na utalii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma