Lugha Nyingine
Rais wa China afanya ukaguzi mkoani Qinghai
Rais Xi Jinping wa China, amefanya ukaguzi katika Mkoa wa Qinghai, Kaskazini Magharibi mwa China Juni 18, ambapo alitembelea Shule ya Sekondari ya Makabila ya Guoluo Xining na Hekalu la Hongjue mjini Xining.
Kwenye ukaguzi mkoani humo, Rais Xi amefahamishwa kuhusu juhudi za mkoa huo katika kuendeleza kazi ya elimu kupitia ushirikiano kati ya sehemu za mashariki na magharibi za China, na kupitia kila sehemu ya mashariki isaidie kazi ya elimu ya sehemu moja ya magharibi.
Rais Xi pia amefahamishwa kuhusu juhudi zilizofanywa katika utoaji mafunzo kuhusu uelewa wa pamoja wa Taifa la China, na waumini wa dini ya Kibudha ya Kitibet kutukuza mila na desturi nzuri za uzalendo na kupenda dini yake, na nyingine kuhusu kuhimiza mshikamano wa kikabila na kupiga hatua za maendeleo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma