Lugha Nyingine
Chombo kimoja kilichorudi duniani cha Chombo cha Chang'e-6 cha utafiti?wa sayari ya?mwezi chafunguliwa baada ya kuwasili Beijing
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 27, 2024
BEIJING - Chombo kimoja kilichorudi duniani cha Chombo cha Chang’e-6 cha utafiti wa sayari ya mwezi kimefunguliwa kwenye hafla iliyofanyika Beijing siku ya Jumatano alasiri kwenye Taasisi ya Teknolojia ya Anga ya Juu ya China chini ya Kampuni ya Beijing ya Kundi la Sayansi na Teknolojia ya Anga ya Juu la China ambapo watafiti wamefungua chombo hicho na kukagua viashiria muhimu vya kiufundi.
Watafiti wanaohusika na mfumo wa matumizi ya duniani baadaye watafanya kazi inayohusu uhifadhi, uchambuzi na utafiti wa sampuli kama ilivyopangwa.
Chombo hicho ambacho ni kimoja cha Chombo cha Chang'e-6 cha utafiti wa sayari ya mwezi kilitua siku ya Jumanne, kikileta duniani sampuli za kwanza kuwahi kukusanywa kutoka upande wa mbali wa mwezi.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma