Lugha Nyingine
Mji wa Jinhua, Mashariki mwa China wahimiza urithi na maendeleo ya opera ya Wu (5)
Opera ya Wu, ambayo pia inajulikana kwa jina la Opera ya Jinhua, ina historia ya miaka zaidi ya 500. Kwa mara ya kwanza ilikua maarufu katika Mji wa Jinhua na maeneo ya jirani, na ilipewa jina la Wuzhou, ambalo lilikuwa jina la mji huo wa Jinhua katika China ya kale.
Serikali za mitaa za Wilaya ya Jindong katika mji huo wa Jinhua zimekuwa zikitafuta njia bora za kuendeleza urithi na maendeleo ya opera hiyo ya kijadi.
Tangu Machi mwaka huu, mji mdogo wa Lipu katika Wilaya ya Jindong ya Mji wa Jinhua imekuwa ikiandaa maonyesho ya Opera ya Wu katika kumbi za maeneo hayo kila wikiendi, ikiwapa wanakijiji na wapenzi wa Opera ya Wu hali changamani ya kufurahia opera hiyo. Hadi sasa, maonyesho zaidi ya 40 yameshafanyika.
Kijiji cha Zhengdian ni mfano mzuri wa kuendeleza utalii wa kitamaduni wa vijijini. Shughuli kama vile maonyesho ya opera na masoko ya kitamaduni na ubunifu ziliandaliwa, katika juhudi za kutoa jukwaa la maonyesho ya Opera ya Wu na kazi za mikono za kienyeji kama vile michoro ya kubandika kwenye nguo, uchongaji wa tofu na michoro kwa sukari.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma