Lugha Nyingine
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lapitisha azimio kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika ujenzi wa uwezo wa akili mnemba
Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe mosi Julai ulipitisha kwa kauli moja azimio lililopendekezwa na China kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika ujenzi wa uwezo wa akili mnemba (AI), ambalo lilitiwa saini na nchi zaidi ya 140.
Azimio hilo linasisitiza kuwa maendeleo ya akili mnemba yanapaswa kushikilia kanuni za kutoa kipaumbele kwa watu, kutumia akili mnemba kwa nia njema, na kunufaisha binadamu. Linahimiza kwa kupitia ushirikiano wa kimataifa na vitendo halisi kusaidia nchi zote, hasa nchi zinazoendelea kuimarisha ujenzi wa uwezo wao katika akili mnemba, na kuongeza uwakilishi na haki ya kutoa sauti ya nchi zinazoendelea katika usimamizi wa dunia nzima wa akili mnemba.
Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, Fu Cong, alipojulisha mswada wa azimio hilo kwenye mkutano huo alisema kuwa, hivi sasa teknolojia ya akili mnemba imepata maendeleo ya kasi katika dunia nzima, na italeta ushawishi wa kina na wa muda mrefu kwa maendeleo ya jamii na uchumi ya nchi zote na maendeleo ya ustaarabu wa binadamu. Hata hivyo, nchi nyingi, hasa zile zinazoendelea, bado hazijapata fursa ya kutumia kihalisi akili mnemba, au kunufaika nayo. Na pengo la kidijitali duniani linaonekana kuwa linapanuka. Nchi wanachama wengi wa Umoja wa Mataifa wanatarajia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa juu ya ujenzi wa uwezo wa akili mnemba, kuendeleza na kutumia kwa usawa teknolojia ya akili mnemba, na kunufaika pamoja na matunda ya akili mnemba.
Fu Cong alisema kuwa, upande wa China unatarajia kutumia fursa ya kupitishwa kwa azimio hilo, na kujiunga pamoja na nchi wanachama wengi wa Umoja wa Mataifa katika kuhimiza kwa hamasa utekelezaji wa azimio hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma