Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping asifu upekee wa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano kati ya China na Kazakhstan
Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev, Julai 2, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)
ASTANA - Rais wa China Xi Jinping amewasili Astana kwa ajili ya ziara ya kiserikali nchini Kazakhstan siku ya Jumanne, ambapo pia atahudhuria Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO). Katika hotuba yake ya maandishi aliyotoa rais Xi baada ya kuwasili Astana, amesema kwamba China na Kazakhstan zimeanzisha uhusiano wa kipekee wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote ulio wa kudumu.
Rais huyo wa China amesema ana furaha tele kutembelea nchi hiyo nzuri ya Kazakhstan kwa mwaliko wa Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev, na kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, akiongeza kuwa yeye, kwa niaba ya serikali ya China na watu wa China, amewasilisha salamu za dhati na za kutakia kila la kheri kwa Tokayev na watu rafiki wa Kazakhstan.
Rais Xi amesema, urafiki kati ya China na Kazakhstan ulianzia enzi na Dahari. Katika zaidi ya miaka 2,000 iliyopita, Njia ya Kale ya Hariri iliunganisha kwa karibu nchi hizo mbili, ikionesha mwanzo wa historia ya mawasiliano ya kirafiki, amesema.
Katika miaka 32 iliyopita tangu China na Kazakhstan zianzishe uhusiano wa kidiplomasia, uhusiano huo umestahimili majaribio ya nyakati na misukosuko ya mazingira ya kimataifa, uhusiano huo umekuwa uhusiano wa kipekee wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote ulio wa kudumu.
Rais Xi amekumbuka kwamba miaka 11 iliyopita, kwa mara ya kwanza alitoa pendekezo nchini Kazakhstan kuhusu kujenga pamoja wa Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri, na hadi leo, ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kati ya China na Kazakhstan umepata matokeo yenye matunda mazuri.
Ushirikiano wa pande mbili wa kiuchumi na kibiashara umefikia kiwango cha juu zaidi, mawasiliano katika mambo ya utamaduni yamepata matokeo mengi mazuri, na ushirikiano wa mambo ya kimataifa wa pande hizo mbili umekuwa wa karibu na wenye ufanisi, hali ambayo si tu imeboresha ustawi wa watu wa pande hizo mbili, lakini pia imeingiza utulivu na nguvu katika hali ya kimataifa na kikanda, Rais Xi ameongeza.
Amesema katika ziara yake hiyo atakuwa na mazungumzo na Rais Tokayev na kubadilishana naye kwa kina maoni kuhusu uhusiano kati ya China na Kazakhstan, ushirikiano wa pande zote na masuala mengine ya kimataifa na ya kikanda ambayo yanafuatiliwa kwa pamoja, kwa lengo la kuweka mipango na upangaji mpya juu ya maendeleo ya uhusiano wa kipekee wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote ulio wa kudumu wa China na Kazakhstan.
Rais Xi pia amesema anatarajia kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kwa kujadili na pande zote kuhusu mustakabali wa jumuiya hiyo na njia za kuendeleza ushirikiano.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma