超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Rais Xi Jinping akutana na Rais Japarov wa Kyrgyzstan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2024

Rais Xi Jinping wa China akikutana na rais Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan. (Picha na Yin Bogu/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na rais Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan. (Picha na Yin Bogu/Xinhua)

Mchana wa tarehe 3, Julai kwa saa za Kazakhstan, rais Xi Jinping wa China alikutana na rais Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan kabla ya kuhudhuria kwenye mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Astana.

Xi alisema, mwezi Mei mwaka jana tulifanya mazungumzo yenye matunda kemkem huko Xi’an, China, tukifikia maoni mengi ya pamoja kuhusu uhusiano kati ya China na Kyrgyzstan na ushirikiano wa nchi zetu mbili katika sekta mbalimbali. Katika mwaka uliopita, maoni hayo ya pamoja yametekelezwa vizuri, na habari nzuri za ushirikiano wetu zimetokea tena na tena. China ingependa kuona Kyrgyzstan inayopata maendeleo kwa hatua madhubuti, na itaendelea kuunga mkono kithabiti Kyrgyzstan kulinda uhuru wake, mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi yake, na kuiunga mkono kithabiti kutafuta njia ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya nchi yake.

Xi alisisitiza kuwa, pande hizo mbili zinatakiwa kupanua mawazo na kusukuma ushirikiano wa kujenga pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”kwenye kiwango cha juu na kuendelea kwa kina, kupanua ushirikiano katika biashara na uwekezaji, kuinua kiwango cha mafungamano ya mawasiliano, na kuongeza ushirikiano katika nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora.

Rais Sadyr Japarov alisema, ninakumbuka vizuri ziara yangu nchini China mwezi Mei mwaka jana, ambayo ilianzisha zama mpya za uhusiano kati ya Kyrgyzstan na China. Hivi sasa uhusiano wa kisiasa kati ya nchi zetu mbili unaendelea kwenye kiwango cha juu, idara mbalimbali za nchi zetu zinadumisha mawasiliano ya karibu, ushirikiano na mawasiliano kwenye ngazi ya mitaa yanastawi, na uwekezaji na biashara za pande hizo mbili zinaongezeka kwa hatua madhubuti. Katika hali ya kukabiliwa na mabadiliko ambayo hayakutokea katika miaka mia moja iliyopita, siku zote uhusiano kati yetu unadumisha uimara wake kama miamba. Hakuna maoni tofauti ya kisiasa au kizuizi chochote cha ushirikiano kati ya nchi zetu mbili. Upande wa Kyrgyzstan ungependa kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja. Inakaribisha kampuni nyingi zaidi za China kuwekeza Kyrgyzstan na itatoa mazingira mazuri kwa kampuni hizo.

Rais Xi Jinping wa China akikutana na rais Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan. (Picha na Yin Bogu/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na rais Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan. (Picha na Yin Bogu/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha