Lugha Nyingine
Rais Xi atoa?wito kwa China na Russia kuendelea kuimarisha kushabihiana kwa mikakati ya maendeleo
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Russia Vladimir Putin kabla ya Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai mjini Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Ju Peng)
ASTANA - Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumatano alipokutana na Rais wa Russia Vladimir Putin kabla ya Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) mjini Astana ametoa wito kwa China na Russia kuendelea kuimarisha uunganishaji wa mikakati ya maendeleo na uratibu wa kimkakati wa kimataifa.
Rais Xi amebainisha kuwa, Rais Putin alifanya ziara ya kiserikali nchini China mwezi wa Mei, akisema kuwa pande hizo mbili zinashirikiana kukupanga maendeleo ya baadaye ya uhusiano wa pande mbili wakati China na Russia zinaadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia.
“Zikikabiliana na hali ya kimataifa iliyojaa misukosuko na mabadiliko, nchi hizo mbili zinapaswa kuendelea kushikilia matarajio ya awali ya urafiki wa kudumu, na kushikilia azma ya kunufaisha watu wao,” Rais Xi amesema.
Ametoa wito kwa China na Russia kuendelea kudumisha thamani ya kipekee katika uhusiano kati ya China na Russia, na kuchunguza nguvu chochezi za ndani za ushirikiano wa pande mbili, akisema kwamba nchi hizo mbili zinapaswa pia kufanya juhudi mpya kulinda haki na maslahi yao halali na kulinda kanuni za msingi zinazoongoza uhusiano ya kimataifa.
China inaiunga mkono Russia katika kutekeleza majukumu yake ya kuwa mwenyekiti wa BRICS, kushikamana "Nchi za Kusini", kuzuia "Vita baridi vipya" na kupinga vikwazo haramu vya upande mmoja na umwamba, amesema.
Kwa upande wake, Putin amemshukuru Rais Xi kwa kumpokea kwa furaha katika ziara yake ya kiserikali nchini China mwezi Mei, akikumbuka kwamba waliadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Russia na China na kufanya mipango ya maendeleo ya baadaye ya uhusiano kati ya Russia na China.
Kwa sasa uhusiano kati ya Russia na China uko katika ngazi ya juu zaidi ya historia, amesema Putin, akiongeza kuwa pande hizo mbili zinaheshimiana, na kutendeana kwa usawa na kunufaishana.
Pia amesema kuwa uhusiano wa Russia na China ni wa kutofungamana na upande wowote na haulengi upande wowote wa tatu, ambayo inaendana na ustawi wa watu wa nchi hizo mbili.
Akibainisha kuwa hivi karibuni China itachukua nafasi ya uenyekiti wa zamu wa SCO, Rais Putin amesema Russia itaunga mkono kikamilifu kazi ya China na kushirikiana na nchi nyingine wanachama ili kuendelea kuimarisha ushawishi wa kimataifa wa jumuiya hiyo, kulinda amani na usalama wa kikanda.
Ikiwa ni mwenyekiti wa zamu wa BRICS mwaka huu, Russia inatarajia kuimarisha mawasiliano na uratibu na China kuhusu ushirikiano wa BRICS, ameongeza.
Wakuu hao wawili pia wamebadilishana maoni kuhusu masuala ya kimataifa na ya kikanda ambayo yanafuatiliwa na pande zote mbili.
Rais Xi amesisitiza kuwa, China daima iko upande sahihi wa historia, inashikilia kuhimiza mazungumzo ya amani, na ingependa kuendelea kufanya juhudi kwa ajili ya suluhusu ya kisiasa kwa mgogoro wa Ukraine na masuala mengine ya kikanda.
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Russia Vladimir Putin kabla ya Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai mjini Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Ju Peng)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma