超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Rais Xi Jinping akutana na Rais Mirziyoyev wa Uzbekistan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2024

Julai 3 kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais Mirziyoyev wa Uzbekistan kabla ya kuhudhuria Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Astana, Kazakhstan. (Mpiga picha:Zhai Jianlan/Xinhua)

Julai 3 kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China alikutana na Rais Mirziyoyev wa Uzbekistan kabla ya kuhudhuria Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Astana, Kazakhstan.

Rais Xi ameeleza kuwa Mwezi Januari Mwaka huu, Rais Mirziyoyev alifanya ziara ya kiserikali nchini China kwa mafanikio, na tuliamua kupandisha uhusiano kati ya China na Uzbekistan kuwa Uhusiano wa Wenzi wa Kimkakati wa Pande Zote kwa siku zote katika Zama Mpya, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya China na Uzbekistan yenye mustakbali wa pamoja kwenye ngazi ya juu zaidi, ambapo maendeleo ya uhusiano kati ya nchi zetu mbili yameingia katika kipindi kipya. Mwaka huu ni maadhimisho ya mwaka wa 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. China inaharakisha ujenzi wa mambo ya kisasa ya China, na Uzbekistan pia inahimiza kwa pande zote utekelezaji wa Mkakati wa "Uzbekistan-2030". China inapenda kushirikiana na Uzbekistan katika kuhimiza maendeleo ya kiwango cha juu ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili, zikiwa kuzingatia ustawi wa nchi na manufaa kwa watu.

Xi Jinping alisisitiza kuwa China inaunga mkono kithabiti Uzbekistan kulinda uhuru, mamlaka ya nchi na usalama wa taifa, na China ni rafiki na mshirika wa kuaminika wa Uzbekistan. Pande hizo mbili zinapaswa kuhimiza kwa kina ushirikiano wa ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kutekeleza mipango ya muda wa kati na mrefu ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na uwekezaji, kuharakisha ujenzi wa reli ya China-Kyrgyzstan-Uzbekistan, na ushirikiano katika nishati ya jua, nishati ya upepo, magari yanayotumia nishati mpya na nyanja nyinginezo, na kuendelea kuimarisha ushirikiano katika kupunguza umaskini, na usimamizi wa jamii. China inapenda kushirikiana na Uzbekistan katika kuharakisha utekelezaji wa matokeo ya Mkutano wa kilele wa Xi'an kati ya China na Asia ya Kati, kuimarisha uratibu na ushirikiano, na kuhakikisha Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai daima inakua kwa mwelekeo unaozingatia maslahi ya pamoja ya wote.

Julai 3 kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais Mirziyoyev wa Uzbekistan kabla ya kuhudhuria Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Astana, Kazakhstan. (Mpiga picha:Zhai Jianlan/Xinhua)

Julai 3 kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais Mirziyoyev wa Uzbekistan kabla ya kuhudhuria Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Astana, Kazakhstan. (Mpiga picha:Zhai Jianlan/Xinhua)

Mirziyoyev amesema, chini ya uongozi wa busara wa Rais Xi Jinping, China imefanikiwa kukabiliana na hatari na changamoto mbalimbali na kupata mafanikio makubwa ya kuongoza duniani katika sekta za uchumi, sayansi na teknolojia, Uzbekistan inatoa pongezi na kuutakia mafanikio Mkutano wa tatu wa Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China. Uzbekistan inashikilia kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na inapambana kithabiti na "nguvu tatu" za ugaidi, mafarakano na siasa kali, na inapenda kuwa marafiki na washirika wa kutegemeka wa China, kuendelea kuheshimiana, kuelewana, na kusaidiana, na kuhimiza ushirikiano halisi katika sekta mbalimbali ili kupata matokeo zaidi. Uzbekistan inapenda kuratibu na kushirikiana kwa karibu na China katika mifumo ya pande nyingi kama vile Mfumo wa China na Asia ya Kati na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, na kuhimiza utekelezaji wa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia,Pendekezo la Usalama wa Dunia, na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia yaliyotolewa na Rais Xi Jinping. ?

Cai Qi na Wang Yi walihudhuria kwenye mkutano huo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha