超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Xi Jinping aonya nchi wanachama wa SCO juu ya tishio halisi kutoka kwenye mawazo ya Vita Baridi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 05, 2024

Rais Xi Jinping wa China akihudhuria Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kwenye Kasri la Uhuru mjini Astana, Kazakhstan, Julai 4, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

ASTANA - Rais wa China Xi Jinping siku ya Alhamisi wakati akihudhuria Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) ametoa wito kwa nchi hizo wanachama wa SCO kuhakikisha usalama katika wakati wa kukabiliana na tishio halisi kutoka kwenye mawazo ya Vita Baridi.

Amehimiza nchi hizo wanachama kushikilia mawazo ya usalama wa pamoja, wa pande zote, wa ushirikiano na endelevu, kukabiliana na changamoto ngumu zenye utatanishi za usalama kwa kupitia njia ya mazungumzo na uratibu, na kuendelea kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja kwa kukabiliana na mazingira ya kimataifa yanayobadilika kwa kina, ili kujenga Dunia yenye amani ya kudumu na usalama kwa wote.

Rais Xi ameipongeza Kazakhstan, nchi mwenyekiti wa zamu, kwa juhudi zake na mchango mkubwa wake katika kukamilisha utaratibu wa utendaji wa SCO na kuendeleza kwa kina ushirikiano katika sekta mbalimbali, na ameikaribisha Belarus ikiwa mwanachama kuhudhuria kwa mara ya kwanza mkutano huo wa wakuu wa nchi wanachama wa SCO.

Amesema kuwa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ilianzishwa mwanzoni mwa karne hii wakati mapambano na migawanyiko iliyoachwa na Vita Baridi ilikuwa bado haijatatuliwa.

Nchi wanachama waanzilishi wa SCO walifanya uamuzi wa kihistoria wa kutafuta maendeleo ya amani, kuweka dhamira katika urafiki na ujirani mwema, na kujenga aina mpya ya uhusiano wa kimataifa, Rais Xi amesema, akiongeza kuwa "Moyo wa Shanghai" umekuwa mtazamo juu ya thamani ya pamoja na kanuni elekezi kwa nchi hizo wanachama.

Akibainisha kuwa SCO imekuwa na nchi mwanachama wake wa 10 tangu kuanzishwa kwake miaka 23 iliyopita, Rais Xi amesema msingi wa ushirikiano wa SCO umekuwa thabiti zaidi kwani "familia kubwa" ya SCO ina idadi kubwa ya nchi wanachama ambao wanatoka mabara matatu kote duniani.

“Wakati Dunia inakabiliwa na mabadiliko ya kasi ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita, jamii ya binadamu imesimama kwenye njia panda ya historia tena,” Rais Xi amesema.

Amesema kuwa SCO inasimama kwenye upande sahihi wa historia, haki na usawa, na ina umuhimu mkubwa kwa Dunia.

Ametoa wito kwa nchi wanachama wa SCO kulinda haki ya maendeleo katika kukabiliana na hatari halisi ya "ua mdogo, nyuzio ndefu."

“Nchi wanachama wa SCO zinapaswa kuimarisha mshikamano na kupinga kwa pamoja uingiliaji wa nje, na kukabiliana na changamoto halisi za uingiliaji na ufarakanishaji,” amesema.

Viongozi wa nchi wanachama wa SCO waliohudhuria mkutano huo wametathimini na kupongeza mchango wa kiujenzi wa jumuiya hiyo katika kulinda amani na usalama wa kikanda, na wameahidi kuimarisha zaidi ushirikiano katika sekta za biashara, usafirishaji, nishati, mambo ya fedha, kilimo, uchumi wa kidijitali na uvumbuzi wa kiteknolojia, na kuongeza zaidi ushirikiano katika mambo ya elimu, utamaduni, utalii na vijana.

Mkutano huo umeiidhinisha rasmi Belarus kujiunga na SCO, na kuamua kuwa China itaanza tena zamu yake ya nchi mwenyekiti wa jumuiya hiyo kwa Mwaka 2024-2025.?

Rais Xi Jinping wa China akiwa katika picha na viongozi wengine wanaohudhuria Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kwenye Kasri la Uhuru mjini Astana, Kazakhstan, Julai 4, 2024. (Xinhua/Ju Peng)

Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev mjini Astana, Kazakhstan, Julai 4, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev mjini Astana, Kazakhstan, Julai 4, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

Rais Xi Jinping wa China akihudhuria Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kwenye Kasri la Uhuru mjini Astana, Kazakhstan, Julai 4, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China akihudhuria Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kwenye Kasri la Uhuru mjini Astana, Kazakhstan, Julai 4, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha