Lugha Nyingine
Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Hungary
(Picha inatoka Xinhua)
Rais Xi Jinping wa China leo siku ya Jumatatu mjini Beijing amekutana na waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban, ambaye yuko ziarani nchini China.
Rais Xi amesema China na Hungary zinapaswa kudumisha mawasiliano ya viongozi na kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa.
Amesema, nchi hizo mbili zinapaswa kuongeza uratibu na ushirikiano wa kimkakati, kuendelea kuungana mkono, kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kuendelea kuongeza yaliyomo katika uhusiano wao wa wenzi wa kimkakati wa pande zote wa wakati wote, ili kunufaisha wananchi wa nchi hizo mbili.
Rais Xi pia ameipongeza Hungary kwa kuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya, na kusisitiza kuwa uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya una umuhimu wa kimkakati na athari ya kimataifa, unapaswa kuendelezwa vizuri na kwa utulivu, na kukabiliana kwa pamoja na changamoto za kimataifa.
Naye Orban amesema nchi yake inapongeza mchango na ushawishi wa China duniani, na iko tayari kuzidisha ushirikiano na uratibu na China.
Ameongeza kuwa Hungary inashikilia kuimarisha ushirikiano na China, na iko tayari kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma