Lugha Nyingine
China yafikia rekodi ya juu ya usajili wa magari yanayotumia?nishati mpya katika nusu ya kwanza ya Mwaka 2024
Watu wakitazama gari linalotumia nishati mpya lililokuwa likionyeshwa kwenye Maonyesho ya Teknolojia za Akili Bandia Duniani Mwaka 2024 katika Mji wa Tianjin, Kaskazini mwa China, Juni 22, 2024. (Xinhua/Zhao Zishuo)
BEIJING - Magari milioni 4.397 yanayotumia nishati mpya (NEVs) yalikuwa yamesajiliwa kwa mara ya kwanza nchini China katika nusu ya kwanza (H1) ya mwaka 2024, ikifanya idadi ya jumla ya magari hayo yanayoendeshwa barabarani kwa sasa kufikia milioni 24.72 mwishoni mwa Juni, Idara ya polisi ya China imesema.
Idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 39.41 kuliko mwaka jana wakati kama huo. Kwa kulinganisha, magari hayo milioni 3.128 yalisajiliwa katika nusu ya kwanza ya Mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 41.6 kutoka kipindi kama hicho Mwaka 2022.
Hadi kufikia Juni 2024, China ilikuwa na vyombo vya usafiri barabarani milioni 440 vinavyofanya kazi, yakiwemo magari milioni 345. Magari yanayotumia nishati ya umeme pekee ndiyo yanaongoza magari yanayotumia nishati mpya, huku milioni 18.13 yakiwa yanatumika, ikichukua asilimia 73.36 ya jumla ya magari yote yanayotumia nishati mpya, kwa mujibu wa takwimu hizo kutoka polisi.
Zaidi ya hayo, madereva wapya milioni 13.97 walipata leseni zao katika nusu ya kwanza ya Mwaka 2024. Jumla ya madereva wenye leseni nchini China sasa inafikia milioni 532, huku milioni 496 kati yao wakiwa madereva wa magari.
Nchini kote China, miji 96 inajivunia kuwa na magari zaidi ya milioni 1, ikiwa ni ongezeko la miji minane ikilinganishwa na kipindi kama hicho Mwaka 2023. Kati yake, miji 43 ina magari zaidi ya milioni 2, wakati miji 26 ina magari zaidi ya milioni 3.
Hasa, idadi ya magari katika miji ya Chengdu, Beijing, na Chongqing kila mmoja unazidi milioni 6, wakati Shanghai, Suzhou, na Zhengzhou kila mmoja una magari zaidi ya milioni 5.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma