超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Kenya yatafuta ushirikiano na China kupanua maeneo maalum ya viwanda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 17, 2024

NAIROBI - Kenya ina nia ya kushirikiana na China kupanua maeneo yake maalum ya viwanda, Juma Mukhwana, katibu mkuu wa Idara ya Taifa ya Viwanda katika Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda ya Kenya, amesema siku ya Jumanne pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Jotoardhi wa Kenya lililofanyika mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi.

“Tunaiona China kama mshirika anayeweza kutusaidia kustawisha sekta ya viwanda nchini kwa kujenga maeneo mengi maalum ya viwanda,” amesema.

Kwa mujibu wa Mukhwana, mchango wa sekta ya viwanda katika uchumi wa nchi hiyo ulipungua hadi asilimia 7.6 Mwaka 2023 kutoka asilimia 11 Mwaka 2011.

Mkutano huo wa siku mbili umewakutanisha pamoja wataalam, watunga sera, wafadhili, na wawekezaji katika sekta ya jotoardhi kutoka nchi 20 za Afrika ili kuimarisha matumizi ya vyanzo vya nishati mbadala katika bara hilo.

Mukhwana amesema mahitaji ya sasa ya nafasi katika maeneo maalum ya viwanda yaliyopo yanazidi uwezo wa nchi wa kuanzisha maeneo mengi maalum ya viwanda, na Kenya ina nia ya kujifunza mambo muhimu kutokana na mafanikio ya China katika kuendeleza maeneo maalum ya viwanda.

Kenya imejenga maeneo maalum ya viwanda katika kila kaunti 47 za nchi hiyo ambayo yanaweza kutumia malighafi zinazopatikana nchini humo kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zilizokamilika. Kutokana na uungaji mkono wa China, Kenya inatarajia kuwa kitovu cha utengenezaji bidhaa barani Afrika, Mukhwana amesema.

Kenya ina nia ya kushirikiana na washirika wa kimataifa, wakiwemo wawekezaji wa China, kujenga na kuendesha maeneo maalum ya viwanda, amesema, akiongeza kuwa ushirikiano na China unatarajiwa kuvutia wazalishaji kutoka China kuanzisha biashara yao nchini Kenya kwa lengo la kusafirisha kwenye soko la kimataifa.?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha