Lugha Nyingine
Waandaaji wasema Tamasha la ZIFF kuvutia filamu zaidi ya 3,000 kutoka duniani kote
Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF), ambalo pia linajulikana kama Tamasha la Nchi za Majahazi, litakuwa na filamu zaidi ya 3,000 kutoka kote duniani.
Hayo yamesemwa na afisa mtendaji mkuu wa ZIFF Joseph Mwale kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika Jumanne jijini Dar es Salaam.
Amesema tamasha hilo ambalo ni tukio kubwa la kitamaduni la Zanzibar litakalofanyika kuanzia Agosti 1 hadi 4, litavutia watengeneza filamu kutoka nchi 100, zikiwemo China, Tanzania, Ujerumani, Uingereza, Indonesia, Poland, Argentina, Hispania, Brazil, Marekani na nchi nyingine za Afrika.
Tamasha hilo litakalo jumuisha shughuli kama vile maonesho ya filamu na mashindano, warsha, sanaa na maonesho, na kuvutia wageni zaidi ya 200,000 kutoka duniani kote, linalenga kuendeleza na kutangaza tasnia ya filamu na za utamaduni kama kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa kikanda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma