Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping aomboleza kifo cha kiongozi wa Vietnam Nguyen Phu Trong
Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akiomboleza kifo cha Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) Nguyen Phu Trong kwenye Ubalozi wa Vietnam nchini China Julai 20, 2024. (Xinhua/ Shen Hong)
BEIJING - Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), alienda kwenye Ubalozi wa Vietnam nchini China siku ya Jumamosi kuomboleza kifo cha Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) Nguyen Phu Trong ambapo kwenye ukumbi wa maombolezo katika ubalozi huo, ambao mbele yake umewekwa picha ya Trong kulikuwa na mashada ya maua yaliyotumwa na Xi na wajumbe wengine wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi.
Pia kulikuwa na mashada ya maua yaliyotumwa na Kamati Kuu ya CPC, Bunge la Umma la China, Baraza la Serikali la China, Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), Ofisi ya Mambo ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya CPC, Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wizara ya Ulinzi ya China, Kamati ya Chama cha CPC ya Beijing na Serikali ya Mji wa Beijing, na jumuiya husika za watu.
Rais Xi alitembea hadi mbele ya picha ya Trong, akatulia kutoa heshima za kukaa kimya kwa muda kabla ya kuiinamia mara tatu picha hiyo, na akaandika ujumbe wenye saini yake kwenye kitabu cha maombolezo.
Rais Xi akimsifu Trong kuwa mfuasi mwaminifu wa Umarksi na kiongozi mkuu wa CPV na watu wa Vietnam, amesema kuwa Trong alijitoa mwenyewe kikamilifu kwa ajili ya CPV na nchi, kwa watu wa Vietnam na kwa lengo kuu la ujamaa nchini Vietnam, na amekuwa akiheshimiwa na kupendwa na chama, wanajeshi na watu wa Vietnam.
Rais Xi amekumbuka kuwa katika muongo mmoja uliopita, yeye na Trong walikuwa wamedumisha mawasiliano ya karibu na kuendeleza ukomredi wa kina, na kwamba mwaka jana walitangaza kwa pamoja kuinua uhusiano wa pande mbili hadi kuwa jumuiya yenye umuhimu wa kimkakati ya China na Vietnam iliyo ya mustakabali wa pamoja, ambayo ni hatua muhimu katika uhusiano wa pande mbili.
"Kufariki dunia kwa Komredi Nguyen Phu Trong kumetufanya kupoteza mhimiazaji wa uhusiano kati ya China na Vietnam na mshirika kwa mambo ya ujamaa, na tumehuzunishwa sana," amesema Rais Xi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma