Lugha Nyingine
Kampuni ya SAIC-GM-Wuling ya China yarekodi mauzo makubwa ya magari yanayotumia nishati mpya katika Nusu ya Kwanza ya Mwaka huu
Roboti ikifunga vioo vya mbele vya magari kwenye karakana ya teknolojia za kisasa ya kampuni ya kuunda magari ya SAIC-GM-Wuling ya China mjini Liuzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China, Mei 9, 2024. (Xinhua/Jin Haoyuan)
NANNING - SAIC-GM-Wuling (SGMW), ambayo ni kampuni ya ubia ya uundaji magari kati ya kampuni za SAIC Motor, General Motors na Liuzhou Wuling Motors, imerekodi mauzo makubwa ya magari ya nishati mpya (NEV) katika miezi sita ya kwanza ya Mwaka 2024, ikiuza magari 243,000 ya NEV katika kipindi hicho.
Yakichukua asilimia 37.6 ya jumla ya mauzo yote ya magari ya kampuni hiyo ya ubia kuanzia Januari hadi Juni, mauzo ya NEV ya kampuni hiyo yameongezeka kwa asilimia 35.5 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, taarifa ya kampuni hiyo imesema.
Kampuni hiyo pia imerekodi idadi kubwa ya magari yaliyouzwa nchi za nje katika miezi sita ya kwanza mwaka huu, huku ikiongeza kwa asilimia 16 mwaka hadi mwaka na kufikia magari 107,126.
Indonesia ni soko kubwa zaidi la mauzo ya nje ya kampuni hiyo, huku aina tatu za magari yanayotumia nishati ya umeme yakichukua asilimia zaidi ya 60 ya soko lote la NEV la nchi hiyo.
Makao makuu ya kampuni ya SGMW yako katika mji wa Liuzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma