Lugha Nyingine
Rais Xi aagiza Shirika la Ndege la Xiamen kutoa mchango katika mawasiliano ya pande za Mlango Bahari wa Taiwan
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping kwenye barua ya majibu kwa wafanyakazi wa shirika la ndege la Xiamen katika kuadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwake ameagiza shirika hilo kufanya juhudi kubwa zaidi katika kuhudumia maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kuhimiza mawasiliano na ushirikiano katika pande za Mlango-Bahari wa Taiwan.
Xiamen, mji wa pwani wa China Bara upande wa magharibi wa Mlango-Bahari wa Taiwan, uko katika mstari wa mbele wa mawasiliano na mafungamano ya pande za Mlango-Bahari wa Taiwan.
Katika wakati alipokuwa naibu meya wa mji huo, Rais Xi alisaidia Shirika la Ndege la Xiamen kutatua matatizo mfululizo yaliyotokea katika hatua yake ya awali ya kuanza kutoa huduma.
Katika barua hiyo, Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amesema anafurahi kuona kwamba Shirika la Ndege la Xiamen, ambalo lilianza tangu mwanzo kabisa bila chochote, limepata maendeleo makubwa katika miongo minne iliyopita.
Rais Xi ametoa wito kwa wafanyakazi wa shirika hilo kushikilia mageuzi na uvumbuzi, kuongeza uwezo wa kimsingi wa ushindani wa shirika hilo la ndege, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya kusukuma mbele maendeleo ya sifa bora ya usafiri wa ndege za abiria na kuongeza nguvu ya China katika mawasiliano na uchukuzi.
Shirika la Ndege la Xiamen lilianzishwa Julai 1984, ni shirika la kwanza la ndege nchini China kufanya uendeshaji kwa kufuata mfumo wa kisasa. Kwa sasa linaendesha njia za usafiri wa ndege zaidi ya 400 za nchini na za kimataifa, zikihudumia abiria karibu milioni 40 kwa mwaka.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma