Lugha Nyingine
Kampuni za kimataifa zaidi ya 150 zajiandikisha kushiriki Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China
Hafla ya kutia saini Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China (CIIE) ikifanyika katika Kituo cha Kitaifa cha Maonyesho na Mikutano (Shanghai), Novemba 6, 2023. (Xinhua/Fang Zhe)
SHANGHAI – Kampuni za biashara za kimataifa zaidi ya 150 zimejiandikisha kushiriki Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China (CIIE) mjini Shanghai kwa mara ya saba, zikiwa zimeshashiriki maonyesho hayo yote yaliyopita, waandaaji wa maonyesho hayo wamesema siku ya Jumatano.
Hadi sasa, ukubwa wa jumla wa eneo la maonyesho lililotiwa saini kwa ajili ya maonyesho hayo umezidi mita za mraba 360,000, Sun Chenghai, naibu mkurugenzi wa Ofisi ya CIIE, amesema kwenye mkutano na wanahabari.
Amebainisha kuwa mwaka huu utajumuisha eneo maalum la vifaa vipya kwa mara ya kwanza, likilenga kujenga jukwaa la mawasiliano ya kimataifa kwa ajili ya kuendeleza uvumbuzi na maendeleo katika tasnia ya vifaa vipya.
“Ili kuonyesha mambo muhimu ya usafiri wa siku za baadaye, eneo la maonyesho ya magari la mwaka huu litajumuisha waonyeshaji katika maeneo kama vile uendeshaji gari kiotomatiki, uchumi wa anga ya chini na aina mpya za uhifadhi wa nishati kwa magari,” Sun amesema.
Amebainisha kuwa nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 50 yamethibitisha kushiriki katika maonyesho jumuishi ya kitaifa ya CIIE Mwaka 2024, zikiwemo Norway, Benin, Burundi na UNICEF, ambazo zitakuwa zikishiriki kwa mara ya kwanza.
Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China (CIIE) yamepangwa kufanyika Shanghai kuanzia Novemba 5 hadi Novemba 10.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma