Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping asisitiza ujenzi wa mambo ya kisasa katika ulinzi wa mipaka, pwani na anga wa China
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) kwenye kikao kazi cha Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC siku ya Jumanne kabla ya Siku ya Tarehe Mosi ya Jeshi la China, ametoa wito wa kutimiza mambo ya kisasa katika ulinzi wa mipaka, pwani na anga wa nchi, ili kuufanya uwe imara na thabiti.
Rais Xi akiwa kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC na CMC ametoa salamu za Siku ya Jeshi kwa wanajeshi wote walioko kazini, ikiwa ni pamoja na askari wanamgambo na vikosi vya akiba.
Huang Jizhong kutoka Ofisi ya Pamoja ya wanadhimu wa Majeshi ya Kamati kuu ya kijeshi alifafanua kuhusu masuala mbalimbali ya ujenzi wa mifumo ya kisasa ya ulinzi wa mpaka, pwani na anga na kutoa mapendekezo. Wajumbe wa Ofisi ya Siasa kisha walikuwa na majadiliano.
Baada ya kusikiliza ripoti na majadiliano, Xi alitoa hotuba muhimu. Amesema tangu ulipofanyika Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC Mwaka 2012, Kamati Kuu ya CPC imeongoza kazi ya mageuzi makubwa ya kitaasisi na kuongoza mfululizo wa hatua muhimu za ulinzi wa mipaka, anga na bahari.
Rais Xi amesema, “Jitihada hizi zimelinda kwa nguvu mamlaka ya ardhi na haki na maslahi ya baharini ya China, vilevile kulinda haki ya kutekeleza mkakati wa usalama na maendeleo ya nchi". Rais Xi amedhihirisha kuwa ulinzi wa mpaka, pwani na anga wa China unakabiliwa na fursa mpya na changamoto mpya, na akisisitiza haja ya kuimarisha mpango wa jumla na kuongeza uwezo wa ulinzi wa mpaka.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma