超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Xi Jinping ampongeza To Lam kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 05, 2024

BEIJING- Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Jumamosi amemtumia salamu za pongezi To Lam, kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV).

Katika salamu hizo za pongezi, Xi amesema amefurahi kupata habari kwamba To Lam kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam, akiwa kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC na kwa jina lake mwenyewe angetoa mapongezi kwa furaha kubwa kwa To Lam na viongozi wa awamu mpya wa chama cha CPV.

Amesema, katika miaka ya hivi karibuni, CPV imetekeleza misingi ya azimio la Mkutano Mkuu wa 13 wa CPV, kuhimiza kwa nguvu kubwa ujenzi wa chama, na kuhimiza ujenzi wa ujamaa na mambo mbalimbali ya chama cha CPV kupata mafanikio makubwa zaidi.

Xi ameelezea imani yake kuwa chini ya uongozi madhubuti wa Kamati Kuu ya chama cha CPV, chama kizima na watu wa Vietnam watatimiza kwa mafanikio malengo na majukumu yaliyowekwa na Mkutano Mkuu wa 13 wa CPV, kuendeleza kwa kasi maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 14 wa CPV, na kuendelea kusonga mbele kuelekea malengo yaliyowekwa kwa ajili ya miaka mia moja ya CPV na miaka mia moja ya nchi.

Xi amesema kuwa China na Vietnam ni majirani na marafiki wa kijamaa wanaounganishwa na milima na mito, katika ziara yake ya kiserikali nchini Vietnam mwezi Desemba mwaka jana, pande hizo mbili zilitangaza kwa pamoja ujenzi wa jumuiya ya umuhimu wa kimkakati ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja, kuanzisha safari mpya na ukurasa mpya katika uhusiano kati ya vyama na nchi hizo mbili.

Xi amesema angependa kufanya juhudi pamoja na To Lam ili kuongoza ujenzi wa jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja kupata maendeleo halisi, kuenzi kwa pamoja urafiki wa jadi, kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, kuzidisha mawasiliano ya kimkakati, na kuhimiza ushirikiano wenye matokeo halisi, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa pande hizo mbili na kutoa mchango kwa ajili ya amani na mambo ya maendeleo ya binadamu.

Xi amesema anamtakia Lam mafanikio mapya katika wadhifa wake huo tukufu.?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha