超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Viongozi wa Somalia wavitaka vyombo vya usalama kuwa macho huku idadi ya vifo kwenye shambulizi la kigaidi ikifikia 35

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 05, 2024

Picha hii iliyopigwa Agosti 3, 2024 ikionyesha eneo la ufukwe karibu na hoteli ya Lido Beach huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia. (Picha na Hassan Bashi/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Agosti 3, 2024 ikionyesha eneo la ufukwe karibu na hoteli ya Lido Beach huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia. (Picha na Hassan Bashi/Xinhua)

MOGADISHU - Viongozi wa Somalia wametoa wito siku ya Jumamosi kwa vyombo vya usalama vya nchi hiyo kuendelea kuwa makini kufuatia shambulizi la kikatili la kundi la al-Shabab kwenye hoteli maarufu ya Lido Beach View katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu Ijumaa usiku ambapo shambulizi hilo la kujitoa mhanga lililolenga hoteli hiyo limesababisha vifo vya watu takriban 35 na wengine 126 kujeruhiwa, kwa mujibu wa msemaji wa Polisi Abdifitah Aden Hassan.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na Waziri Mkuu Hamza Abdi Barre waliitisha mkutano wa dharura wa usalama mjini Mogadishu kufuatia shambulizi hilo.

Rais ambaye alipokea taarifa fupi kuhusu jinsi magaidi hao walivyovunja vizuizi vya kiusalama katika ufukwe wa Lido amewatakia wale waliojeruhiwa na wamelazwa hospitalini wapate nafuu haraka.

"Shambulizi la kigaidi kwenye Ufukwe wa Lido linaonyesha ukatili wa al-Shabab na uadui wao dhidi ya watu wa Somalia. Serikali imedhamiria kutokomeza kundi hili kutoka nchi nzima," Rais Mohamud amesema katika taarifa iliyotolewa mjini Mogadishu baada ya mkutano huo wa dharura.

Amesema kuwa mafanikio katika vita dhidi ya ugaidi yanategemea uungaji mkono na ushirikiano wa watu wa Somalia. Rais huyo ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama huku wakiungana ili kutokomeza kundi la al-Shahab nchini humo.

Shambulizi hilo jipya ambalo kundi la al-Shabab limedai kuhusika kupitia redio yake rasmi ya pro-Shabab, likidai kuwa limeua watu 54, lilianza saa 4 usiku kwa saa za huko, siku ya Ijumaa wakati mshambuliaji wa kujitoa mhanga alipolipua kifaa cha kulipuka kwenye lango la kuingilia Lido Beach View.

Washambuliaji wengine watano walivamia eneo ambalo wakazi wengi walikuwa ama wakila chakula, kuogelea au kufanya matembezi.

Aden, msemaji wa polisi, amesema vikosi vya usalama baadaye vilipambana na wapiganaji hao na kuwaua washambuliaji wote katika eneo la tukio na kumkamata mwingine aliyekuwa akiendesha gari lililokuwa na vilipuzi.

Aden amesema, askari mmoja ameuawa na mwingine amepata majeraha wakati wa kurushiana risasi.

Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki (IGAD), imelaani vikali shambulizi hilo baya dhidi ya sehemu inayokaribishwa na kuzungukwa na hoteli na migahawa ya ufukweni, ambayo inapendwa sana Wasomali wengi.

Wachambuzi wanasema shambulizi hilo la al-Shabab kwenye maeneo ya mapumziko ya ufukweni linathibitisha kuwa kundi hilo kigaidi limedhamiria kurejesha utawala wake katika mji mkuu huo wa Somalia baada ya kudhoofishwa na wanajeshi wa Umoja wa Afrika.?

Picha hii iliyopigwa Agosti 3, 2024 ikionyesha eneo la ufukwe karibu na hoteli ya Lido Beach huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia. (Picha na Hassan Bashi/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Agosti 3, 2024 ikionyesha eneo la ufukwe karibu na hoteli ya Lido Beach huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia. (Picha na Hassan Bashi/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha