Lugha Nyingine
Majengo ya Nyumba ya Ganlan: Mtindo wa kipekee wa makazi ya watu wa kabila dogo la Wazhuang wa China
Kijiji cha Pingliu katika Wilaya ya Longlin, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China chenye historia ya zaidi ya miaka 200, ni kijiji kidogo cha watu wa kabila la Wazhuang ambacho kinapakana na mikoa jirani ya Yunnan na Guizhou.
Miongoni mwa mila na desturi na mavazi vilivyohifadhiwa vizuri vya kabila hilo dogo la Wazhuang, ni makazi ya nyumba za kienyeji, nyumba za Ganlan, ambazo ni miundombinu ya makazi ya nyumba zilizojengwa kwa mbao, ni zenye mwonekano wa kipekee zaidi.
Nyumba hizo zinahimiliwa kwa nguzo za mbao, kwa kawaida kila nyumba ina ghorofa tatu na paa za mteremko. Ghorofa ya kwanza, chini hutumiwa sana kama vibanda vya mifugo, wakati ghorofa ya pili na ya juu ni ya familia kuishi na kuhifadhi nafaka mtawalia. Nyumba hizo zilijengwa juu ya ardhi, zinasaidia kuzuia unyevu, kuongeza uingizaji hewa na kuleta mwanga katika nafasi ya kuishi watu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma