Lugha Nyingine
Ukanda wa utamaduni wa China na Cambodia waingiza msukumo katika utalii wa kikanda (2)
SIEM REAP, Cambodia - Ukanda wa Utamaduni wa China na Cambodia umezinduliwa siku ya Jumanne kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Angkor wa Siem Reap, kaskazini-magharibi mwa Cambodia, ukiingiza msukumo mpya kwenye maendeleo ya utalii wa kikanda.
Ukiwa na kaulimbiu ya " Urithi wa Dunia Uso kwa Uso, Kufunzana kati ya Ustaarabu Mkono kwa Mkono," ukanda huo wa utamaduni unalenga kuhimiza zaidi uanuai wa utamaduni na mali ya urithi wa nchi hizo mbili kwani mwaka 2024 ni mwaka wa mawasiliano kati ya watu wa China na Cambodia.
Hafla ya uzinduzi wa ukanda huo imefanyika kwenye sehemu ya abiria wa kimataifa kusubiri ndege katika uwanja huo wa ndege, ikionyesha baadhi ya picha 100 za kupendeza za China na Cambodia pamoja na nchi nyingine za Eneo la Lancang-Mekong. Watembeleaji wanaweza pia kufurahia maonyesho yanayojikita katika mambo matatu ya "udarizi", "uchongaji" na "rangi", yakionyesha mali ya urithi wa utamaduni usioshikika wa Mkoa wa Yunnan kusini magharibi mwa China na Cambodia.
Katika hafla hiyo, Mpango wa Ziara ya Mali ya Urithi wa Dunia, chini ya kaulimbiu ya "Tazama Maeneo 10 ya Urithi wa Dunia katika Siku 10", pia ulizinduliwa.
Chhean Leang, waziri wa nchi katika Wizara ya Habari ya Cambodia, amesema ukanda huo ni hatua nyingine muhimu katika mawasiliano kati ya watu na ya kitamaduni kati ya nchi hizo mbili.
“Ukanda huu wa Utamaduni utaongoza watalii kutoka sehemu mbalimbali za dunia hadi kwenye urithi wa kitamaduni na mandhari ya kipekee na ya kupendeza ya Cambodia na China pamoja na nchi nyingine za Lancang-Mekong kupitia maonyesho ya maeneo ya Mali ya urithi wa dunia na Vitu vya urithi wa utamaduni usioshikika miongoni mwa mengine,” amesema kwenye hafla hiyo.
Wang Jianghong, naibu mkuu wa Idara ya Utamaduni na Utalii ya Mkoa wa Yunnan, amesema ukanda huo umezinduliwa baada ya Mfululizo wa Shughuli za Kitamaduni za China (Yunnan) na Cambodia kuhusu "Kutembelea Maeneo ya Mali ya Urithi ya Yunnan na Angkor" kuzinduliwa mwezi Juni mwaka huu ili kuendeleza utalii wa kihistoria na mali ya urithi wa utamaduni katika pande zote mbili za Yunnan na Cambodia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma