Lugha Nyingine
Uvunaji wa msimu wa kwanza na upimaji mazao ya mpunga unaozalishwa?kwa kujirudia tena kwenye shamba linalojiendesha bila binadamu huko Yiyang, Mkoani Hunan, China
Jumatano, Agosti 7, Jumuiya ya Mazao ya Mkoa wa Hunan wa China iliandaa wataalam kufanya upimaji wa mazao ya uzalishaji wa msimu wa kwanza wa mpunga unaoweza kuzalisha mazao kwa kujirudia tena katika Shamba la Linalojiendesha Lenyewe Bila Binadamu la mpunga unaoweza kuzalisha mazao kwa kujirudia tena katika Eneo la Datonghu la Mji wa Yiyang, Mkoa wa Hunan. Kwa mujibu wa tathmini ya kundi la wataalam hao, kiasi cha mavuno ya eneo hilo la majaribio ya mpunga unaoweza kuzalisha mazo kwa kujirudia tena katika msimu wa kwanza kitafika kilo 754.28 kwa mu.
Shamba Linalojiendesha Lenyewe bila Binadamu la mpunga unaoweza kuzalisha mazao kwa kujirudia tena katika Eneo la Datonghu lilianzishwa mwaka 2023. Shamba hilo linaweza kufanya uanzishaji na udhibiti wa mbali wa kazi za uendeshaji wa mashine za kilimo, kutumia jukwaa la teknolojia za kisasa la kilimo kukamilisha ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu za uzalishaji mpunga katika mchakato mzima, ufanyaji maamuzi wa kisasa wa maelekezo ya kilimo na utekelezaji wa kisasa wa kazi za mashine za kilimo, ambazo zinaweza kufanya miche ya mpunga wa aina hiyo kuanza kuota tena katika msimu wa pili wa kuzalisha mpunga kwa kujirudia tena na kuboresha uzalishaji na ubora wa mpunga unaoweza kuzalishwa kwa kujirudia tena.
(Mpiga picha:Chen Zhenhai/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma