Lugha Nyingine
Chang ashinda medali ya dhahabu ya kwanza kabisa ya China ya mchezo wa ndondi kwa wanawake katika Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024
PARIS - Bondia wa China, Chang Yuan amefanikiwa kupata medali ya dhahabu ya mchezo wa ndondi kwa mabondia wanawake wenye uzito wa kilo 54 kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris siku ya Alhamisi usiku katika uamuzi wa wazi kwa kauli moja dhidi ya Hatice Akbas wa Uturuki ambapo medali hiyo ya dhahabu ya Chang inamaanisha kuwa taji la kwanza kabisa la China katika mchezo wa ndondi kwa wanawake la Olimpiki.
Chang alianza kurusha ngumi nyingi zaidi mfululizo katika raundi ya pili ili kushinda pointi katika raundi mfululizo. Kwa mara nyingine tena, Chang kwa ustadi alitumia ngumi zake kupenya hali ya kujihami ya Akbas kwa kuwa na kasi kali ndani ya ulingo. Mchezaji huyo wa Uturuki alijitahidi kustahimili shinikizo hilo, na kugeukia kushikana mikono ili kujaribu kusimamisha kasi ya Chang.
Baada ya jina lake kuitwa mshindi, Chang alibebwa juu na kocha wake huku wengine wa timu ya China waliokuwa kwenye umati wakishangilia pamoja naye.
Kwenye nusu fainali mchezo huo wa ndondi kwa wanawake wenye uzito wa kilo 75, Li Qian wa China alijitokeza kwenye raundi aliyokuwa amezidiwa awali dhidi ya Caitlin Parker wa Australia na kushinda kwa uamuzi wa kauli moja. Mchezaji huyo wa China alianza polepole na kumruhusu Parker kuingia ndani ya safu yake na kupata pointi nyingi katika raundi ya kwanza.
Hata hivyo, Li alirejea na kulipiza kisasi katika raundi ya pili na nyingine mfululizo zilizofuata na kudumisha usahihi wake wa hali ya juu ili kupata nafasi yake katika pambano litakalofuata la kuwania medali ya dhahabu.
Li atamenyana na Atheyna Bylon wa Panama katika fainali, ambaye amemshinda Cindy Winner Djankeu Ngamba wa timu ya Wakimbizi ya Olimpiki katika mashindano awali kwa pointi 4-1.
Kwenye fainali ya mchezo huo wa ndondi kwa wanaume wenye uzito wa kilo 51, Hasanboy Dusmatov ameshinda medali ya pili ya dhahabu ya Uzbekistan ya mchezo wa ndondi, akimshinda Billal Bennama wa Ufaransa kwa uamuzi wa kauli moja.
Mwanzoni mwa usiku wa jana Alhamisi kwenye nusufainali ya mchezo huo wa ndondi kwa wanaume wenye uzito wa kilo 57, Abdumalik Khalokov alimshinda Charlie Senior wa Australia katika uamuzi wa kauli moja.
Mpiganaji huyo wa Uzbekistan alishinda kwa ufanisi kila kipengele kwenye takriban kila kadi ya alama. Khalokov atamenyana na Munarbek Seiitbek Uulu wa Kyrgyzstan, ambaye amemshinda Javier Ibanez Diaz wa Bulgaria kwa pointi 4-1.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma